Mazoezi ya Kuapishwa Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli Yapamba Moto Dar‏...Angalia Picha Hapa


Kibanda cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Maofisa mbalimbali wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi watakavyokaa wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo
Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo.
Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa Jukwaa Kuu wakati wa maandalizi hayo.
Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na Bendi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa maandalizi hayo.
Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo.

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Fanyeni yote lakini haina baraka wala tija mungu atalipa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dua la kuku-----------------------

      Delete
  2. Inashangaza,ukistaajabu ya musa utaona ya firauni

    ReplyDelete
  3. Watu wazima hovyo Msikae maofini
    Shame you CCM yote kusubiri vyeo magufuli toa toa takataka zote hizi kazi kupokea na kusindikiza kila leo

    ReplyDelete
  4. Mkuu WA mkoa naye anapiga saluti kwani mwanajeshi, Polisi au ndo kuomba ulaji kwa mtoto mdogo magufuli kisa rais
    Shame you mtu mzima hovyo

    ReplyDelete
  5. jee kwenye sherehe hii muhimu atahudhuria rais wa zanzibar dr ally mohamed shein,wananchi tuna hamu ya kumuona.la pili kwa kuwa uchaguzi wote ulifutwa zanzibar na jecha,jee sherehe hii ni ya tanzania bara pekee? tatu muundo wa baraza la mawaziri pia huwahusisha zanzibar,safari hii kule hakukua na uchaguzi jee watashiriki vipi siasa kuu ya kuhusu muungano?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa mujibu wa sheria zanzibar hakuna rais kwa kua muda wake ulishaisha, Dr Shein ni kiongozi wa muda adi pale kitakapo eleweka. Na kwakua matokeo ya uchaguzi yote ya zanzibar yamefutwa basi rais atakae apishwa sasa hivi mimi sifahamu ni wa nchi gani. Na pindi zanzibar watakapo rudia uchaguzi pia sijui watachagua rais wa nchi gani hali yakua kuna rais amesha apishwa? Kutokana na mwenendo wa mambo yanavyokwenda hapa kuna maswali mengi sana ambayo yanahitaji majibu ya dharura kabla hatujafika mbali.

      Delete
  6. Nani amenuna?? Nauliza tena kuna mtu yoyote amenuna??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbowe,kingunge,sumaye,Lowasa,Regina,linda,wolper mmmmmmmmmmmh nimechoka kutaja maana wengi.

      Delete
    2. Hakuna aliye nuna mkuu, bali wananchi wapo ktk msiba ama huoni hali halisi ya wananchi wengi walivyokatishwa tamaa na matokeo ya uchaguzi na kinachoendelea zanzibar?

      Delete
  7. Angalia picha vzr RC hapigi saluti. Ni mwanajeshi aliyepo pembeni ndiye apigae saluti.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sorry nimeona lakini wanafanya nini hapo kila siku kusindikiza na kupokea rais
      Nategemea magufuli hawi wasco dagama

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad