Membe: Tulikuwa Tunagongana Angani Utadhani Nyumbani Kuna Moto

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amempongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwa kupiga marufuku safari za nje ya nchi, akisema mawaziri na watendaji wa Serikali walikuwa wakigongana angani na ndege utadhani Tanzania ilikuwa ikiwaka moto.

Mbunge huyo wa zamani wa Mtama alisema uamuzi huo utaokoa fedha nyingi za Serikali na kumtaka Rais kushusha rungu hilo hadi kwenye mashirika.

Wakati Membe akieleza hayo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alisema kila safari ya nje ina gharama yake na kila safari itakayofutwa zitapatikana fedha kusaidia masuala mengine ya maendeleo katika jamii.

Juzi, Dk Magufuli alipiga marufuku safari za nje ya nchi kwa watendaji na kwamba shughuli ambazo wangekwenda kuzifanya, kuanzia sasa zitahitaji kibali kutoka kwake au zitafanywa na mabalozi wa Tanzania walioko katika nchi husika.

Jana Membe alisema: ?...Tulikuwa tunagongana huko hewani utadhani huku nyumbani kunaungua moto. Tunapobaki huku ndani tunaokoa hela nyingi na nina hakika (Dk Magufuli) ataingilia hata kwenye mashirika. Kuna wakuu wao wanasafiri kila siku, nina hakika wataguswa katika hili. Lazima kuziokoa pesa za kufanyia shughuli nyingine mimi naunga mkono mia moja kwa mia hili.?

Alisema kitendo cha Rais Magufuli kufuta safari za nje hakina maana kwamba uhusiano wa Tanzania na nchi hizo unakufa. ?Hajakataza wageni, wafanyabiashara wa dunia wala wawekezaji kuja Tanzania, hata wawekezaji hawawezi kukataa kuja Tanzania waache gesi, dhahabu, almasi au tanzanite.?

Alisema wapo watu wanaodhani kuwa kauli ya Rais Magufuli itamhusu hadi Waziri wa Mambo ya Nje ?... atakwenda nje maana ukishamuita waziri wa mambo ya nje lazima aende nje. Dk Magufuli hawezi kusema hivyo. Hutasikia amekatazwa maana ndiyo wizara yenyewe na inashughulika na dunia.?

Alisema kauli hiyo pia haina maana kwamba Wizara ya Mambo ya Nje imefutwa kwa kuwa balozi za Tanzania zilizopo nje zipo chini ya wizara hiyo.

CHANZO: Mwananchi

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kikwete na genge la wenzie ndo wamehiaribu hii nchi bora lilivyondoka

    ReplyDelete
  2. Mnafiki mkubwa,kwa nini hukusema haya kabla?hela ilikuwa tamu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hana tofauti na Lowasa na Sumaye, Kingunge n.k. baada ya kuihama CCM ndio wakasema eti CCM haijafanya chochote...........

      Delete
    2. Kwa heshima na taadhima, ni bora unyamaze tu mzee, walimwengu hatutakuelewa

      Delete
  3. Pole sana Mh Membe now is too late pesa nyingi zimeugua moto kama ulivyosema. ulikuwa wapi kumshauri mheshimiwa kumwambia nyumbani hakuna moto. Mbona Magufuli hajaugua moto kwa siku hizi chache alizokaa ikulu? au mlikuwa na jambo lenu ndio maana kila waziri anaghorofa la nguvu....

    ReplyDelete
  4. Ndio shida ya wa bongo kama yeye mnafiki lowasa je? Ndumi la kuwili au?

    ReplyDelete
  5. Membe
    Omary Mjenga yupo wapi swahiba wako mwenye asilimia ya Kenya
    Ukampa naibu balozi Dubai
    Pesa uchaguzi hizo chezea wakenya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad