Mgogoro wa Zanzibar Watua IKULU ya Marekani

Na Swahilivilla, Washington
Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).


Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar.

Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika.

"Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwingine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana Ali.

Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"

Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema;
 
"Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru"
 
Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwenye Umoja wa Mataifa.

Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maneno kama vile "Mshindi wa uchaguzi atangazwe", "maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe", "bila haki hakuna amani' na mengineyo.

Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai "tunataka matokeo yetu ya uchaguzi.."

Akizungumza na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo alisema "Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono Wazanzibari katika kudai haki yao"

Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar.

Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.

Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAYA MATATIZO YA ZANZIBAR NI YA WATANZANIA ITAKUAJE YANAKWENDA MAREKANI

    WATANZANIA NDIO WATAAMUA NA SIO MAREKANI JAMANI MUWE MAKINI HUYO MAALIMU

    SAIF HANA LOLOTE NI TAMAA YA MADARAKA UCHAGUZI UTARUDIWA NDIO ITAJULIKANA NANI MSHINDI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aiseh...we jamaa ni mpumbavu sana
      Kaa kimya

      Delete
  2. WEWE KAMA HAUTAKI UCHAGUZI URUDIWE INA MAANA ULISHINDWA UCHAGUZI WA KWANZA

    NA NINA IMANI UCHAGUZI WA PILI CCM WATASHINDA

    ReplyDelete
  3. WAZANZIBARI HASA WAPEMBA NI WABAGUZI. BORA WAFUKUZWE WARUDI KWAO UARABUNI

    ReplyDelete
  4. Wee unanichekesha mdau,hv unadhani wapemba wana shida ya tanganyika walishasema zamani Wanataka zanzibar yao,Lkn ccm ndo kinganganizi,Nahao walopeleka malalamiko ikulu ya marekani c wamarekani ni watanzania waishio arekakani

    ReplyDelete
    Replies
    1. WAPEMBA ZANZIBAR SIO KWAO SAWA NA MAKABURU WA SOUTH. SO WAFUKUZWE WANATUARIBIA NCHI YETU

      Delete
    2. Wanadai zanzibar yao walimkabizi nani mpaka waidai

      Delete
  5. Nyote hapo juu ni watu musio jielewa Leo hii maalimu selfu amekuwa mlafi wa madaraka na c sheni kweli muna chekesha katiba inasemaje Na mbona wameivunja katiba na kuwa madarakani nan mlafi wa madaraka hapo pumbavu shame on you

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wapemba kaeni chonjo nchi hii haiwahusu

      Delete
  6. KWELI MANENO YAKO WAPEMBA WAFUKUZWE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad