Mikwara ya Marais wa Tanzania Mara Waingiapo Madarakani

Binafsi sikuwepo wakati Nyerere anaingia madarakani, ila hawa wengine kidogo nina kumbukumbu.

Mzee Mwinyi kipindi anaingia madarakani aliazimia kuwafyeka wabadhirifu wote waliopo serikalini, mpaka akapewa fagio la chuma kama ishara ya kuhakikisha wala rushwa na wabadhilifu hawamzidi nguvu. 1995 wakati anatoka madarakani nchi ilikuwa na wala rushwa na wabadhilifu maradufu ya alipoingia, madawa ya kulevya , maana ukwepaji wa kodi na wizi wa rasilimali za nchi hii ulishamili sana kipindi cha mwinyi.

Ben Mkapa aliingia na madarakani akiwa mnyenyekevu kupita maelezo, nakumbuka alishawahi kutoa zuria alilotandikiwa kuonyesha kwamba alikuwa akijishusha na kutotaka makuu, vilevile alipiga marufuku watangazaji wa redio tanzania waliokuwa wameanza kumwita mtukufu kila wanapomtaja. Aliwapachika jina mawaziri wake kuwa ni askari wa myamvuli kuonyesha kwamba amechagua baraza bora kabisa kuwahi kutokea. Matokeo yake yaliyowakuta mawaziri wake wake akina prof mbilinyi, idd simba na wengine hayasemeki. Mkapa ndiye raisi aliyetumia ubabe kutawala, alitoka madarakani akiwa jeuri na mwenye dharau, kipindi chake watu wengi waliuwa na polisi kwa kisingizio cha fujo.

Kikwete yeye alijigamba sana kufunga wala rushwa na alijitanabaisha kuwa uraisi wake hana ubia na mtu . Matokeo yake mikataba mibovu na rushwa kubwa zimeibukia kwake,

Sasa Magufuli ameanza ni mikwara kibao, unadhani ni nini kitatokea?

By gollocko./Jamii Forums
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. SAFARI HII WAMEKUJA NA MKWARA WA PUSHAP NDIO SERA YA AWAMU TA 5.

    ReplyDelete
  2. Nimesikia wakisema eti hapa kazi tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kunyweni ndimu kama hamtaki hapa kazi tu kaeni na raisi wenu wa ukanda huko nyumbani tumemuelewa magufuli anawatumikia watanzania wote bila kujali itikadi ukabila wala dini hapa kazitu kapige ukuta kama umekasirika

      Delete
    2. Yatakushinda,"Hapa Kazi Tuu" Kwa Mtaji Upi Ulionao

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad