Mke wa Deo Filikunjombe Ampigia Kampeni Mdogo wa Filikunjombe Achukue Ubunge Jimbo Aliloliacha Mmewe..Adai Wengine Msiwasikilize Hawana Hata Mahali pa Kufikia Ludewa

Tanzania bado iko kwenye majonzi baada ya msiba wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa,Deo
Najua kuna watu walikuwa na maswali juu ya atakayewaongoza wakazi wa Ludewa, sasa leo Novemba 5, 2015 mke wa marehemu Deo Filikunjombe ‘ Saraha’ ameyaandika maneno haya kupitia akaunti yake ya instagram kuhusiana aliyeteuliwa kugombea jimbo la Ludewa.

Nawaombeni wana ludewa wote kwa heshima nawaomba niwaambie ukweli kuwa huyu ndie anayeweza kuvaa viatu vya mume wangu mpendwa kwani mara nyingi amewahi kumchangia kaka yake ada za watoto tuliokuwa tunawasomesha huko ludewa naombeni msidanyike na maneno ya hao wagombea wengine mbona leo ndo wamekuja ludewa walikuwa wapi kujakuleta maendeleo mpaka iwe baada ya deo kufariki kati ya wagombea wote hakuna rafiki wa mume wangu’ – Saraha
‘hata mmoja tena kwa macho yangu nimewaona wakipewa misaada walete Ludewa na hawakufikisha na mara nyingi amelalamika na kuwaomba jamani tupeleke maendeleo nyumbani hakuna aliesikia hata mmoja ndo maana hawana nyumba ya kufikia matokeo yake wanawaomba kura ilingali hata hawana pakufikia wamefikia nyumba ya kulala wageni mkitaka kumwona mbunge mta mkuta wapi tuwemakini Deo amefanya mengi mpeni mdogo wake amalizie aliyoahidi asanteni sana wanaludewa niwaganili sana mdalikhe sana ccm hoyeeeeeeechagua ccm chagua Philipo filikunjombe hapa kazi tu’ – Saraha

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani tupo kwenye utawala WA kifalme hadi mrithishane ndugu kiti cha ubunge, yeyote aweza kuleta maendeleo ludewa, na kuwa mdogo WA filikunjombe haimaanishi kuwa ndo atakua na roho kama ya filikunjombe, na ikumbukwe kuwa ili uwe mbunge Ni lazima uwe mtanzania bila kujali umetokea Tanzania sehemu gani, hivyo Tulia acha wanaludewa waamue kelele za nini.

    ReplyDelete
  2. Makubwa, umeanza lini siasa bibiwewe, siku zote ulikuwa wapi kupiga hizo kampeni, mbona hapo nyuma hatukukusikia? Mtu yeyote anayekubalika na aongoze ludewa.

    ReplyDelete
  3. Salah unajidhalilisha siasa umeanza lini au unataka watu waanze kukuvua nguo achana na mambo ya siasa au unadhani hatujui maovu yako, tulia mwanamke ulee watoto wako

    ReplyDelete
  4. "kwani mara nyingi amewahi kumchangia kaka yake ada za watoto tuliokuwa tunawasomesha huko ludewa"...., mliokuwa mnawasomesha au aliokuwa anawasomesha mumeo akiwa kama mbunge??? Na mbona mumeo hakuwahi kutamka kuwa Ada hizi nazowasaidia watoto hawa tumechanga Mimi na mdogo wangu, au na Mke wangu? Badala yake alidonate yeye kama mbunge. Achana na siasa wewe sio mwanasiasa Sarah, siasa waachie wenyewe wenye siasa zao, acha kusaka umaarufu. Kinguvu Una madhara yake, shauriyako

    ReplyDelete
  5. Kuna mtu alifanya mengi kama Baba WA Taifa kwa Tanzania yetu? Lakini mbona hakukabidhi madaraka kwa familia yake kisa kafanya makubwa. Basi na mjifunze kutoka kwake, sio lazima ludewa iwakilishwe na ndugu WA deo eti kisa aliifanyia makubwa ludewa, kwa hiyo unataka wanaludewa walipe fadhila kwa kumrithisha mdogo mtu? Mi sioni kama ina mantiki hiyo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad