Mtandao wa TACCEO Walaani Polisi Kuvamia Kituo Chao Kuwakamata Waangalizi na Vifaa Walivyokuwa Wakitumia Kupokea Taarifa

Mtandao wa Asasi za Kiraia za Uangalizi wa Chaguzi (TACCEO), umelaani kitendo cha Polisi kuvamia kituo chao na kuwakamata waangalizi na vifaa walivyokuwa wakitumia kupokea taarifa zilizokuwa zikihusiana na mchakato wa uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mtandao huo umeitaka Polisi kufanya kazi zake kwa weledi, huku ikichukua hatua stahiki kushughulikia suala hilo ikizingatia kuwa kazi ya uangalizi wa uchaguzi ni endelevu.

Kaimu Mwenyekiti wa TACCEO, Hebron Mwakagenda (pichani) alisema kitendo hicho ni ukiukaji wa sheria kwa kuwa waangalizi hao walikuwa wakifanya kazi yao kwa kufuata misingi iliyowekwa kikatiba sambamba na kuzingatia taratibu zote za kisheria.

Mwakagenda alisema kuwa uvamizi huo ulikuwa na lengo la kudhoofisha ustawi wa demokrasia nchini na kuwatisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mambo yanayohusu mchakato wa uchaguzi.

Ni wazi uvamizi huu una lengo la kudhoofisha demokrasia na kuingilia kazi za asasi za kiraia kushiriki kikamilifu katika uangalizi wa uchaguzi hapa nchini,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, TACCEO imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kuthibitisha uhalali na uwapo wa nafasi, haki na wigo wa uangalizi wa uchaguzi nchini.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 29, mwaka huu na polisi walifika kwenye ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilichopo Mbezi, Dar es Salaam na kuwakamata watendaji 36 kwa kosa la kukusanya taarifa za uchaguzi zisizo rasmi.

Katika tukio hilo kompyuta 24, kompyuta mpakato tatu, simu 25 za ofisi na nyingine za waangalizi hao zilikamatwa.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wanaokamatwa na polisi ni wasio na hatia. Wanaotetea uhuru wao na haki za binadamu. Lakini polisi ndio wavamizi. Je JK wewe kama kamanda unayetoka, huoni haya. Je ni amri toka kwako. Je si uhaini huu.Mbona unawachanganya Wananchi kuhusu kazi za upolisi. Je Polisi wanahaki ya kupora, kunyanyasa na kupiga watu?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad