Mwakyembe Azungumzia Tetesi za Yeye Kuwa Waziri Mkuu

Mbunge Mteule wa Jimbo la Kyela,  Dkt. Harrison Mwakyembe (pichani) amesema Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania atatokana  na uteuzi utakaoidhinishwa na  Bunge na si taarifa zilizopo sasa katika mitandao ya kijamii.

Dkt. Mwakyembe ambaye amewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi,  Waziri Mkuu anateuliwa na Rais ambaye huwasilisha jina hilo kwa Spika wa Bunge na baadaye kupigiwa kura na Wabunge.

 Mbunge huyo aliyasema hayo jana Jumapili  (Novemba  15, 2015) Mjini Dodoma wakati alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu tetesi zilizopo katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhusiana na jina lake kutajwa kuwa ndiye Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Mimi siwezi kuwasemea wananchi na siwezi  kusema kuna watu wengi wanasema hivi,  kwani nafasi ya Uwaziri Mkuu haiji kwa njia ya kura ya maoni, wala kwa  njia ya mitandao ya kijamii ni nafasi ya uteuzi inayoidhinishwa na bunge na ni mamlaka ya Rais wa nchi” alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha, Mhe. Mwakyembe aliwataka Watanzania bila kujali itikadi za dini na vyama vyao wamuombee Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuchague viongozi watakao wajibika na ambao wataendana na kasi ya Mhe. Rais.

Wabunge wengine waliotajwa kuwepo kwa uwezekano wa kuteuliwa nafasi ya Uwaziri Mkuu wa Awamu ya Tano ya Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli ni pamoja na Mhe. William Lukuvi, Mhe.  Prof. Sospeter Muhongo na Mhe. January Makamba.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Mwakyembe ndiye kwa mikono yako ulimnunua dr.slaa na akawa MUASI,HAINI NA MSALITI.ALIIKIMBIA NCHI,UNAJUA ALIPO maskini babu wa watu hata kura hakupiga,yeye na hawala yake.wewe mwakyembe ndiye adui nambari moja wa UKAWA,NARUDIA ADUI NAMBARI MOJA.SASA UKITEULIWA HUO MOTO WA UKAWA BUNGENI UTAMFANYA MHESHIMIWA MAGUFULI AKUONDOE TENA HARAKA.NI MSUKOSUKO WA KISIASA JUU YA MSUKOSUKO.HAUFAI MWAKYEMBE.kule kyela kesi ya uchaguzi inakusubiri.haufai mwakyembe.

    ReplyDelete
  2. LUKUVI SAWA,HAWA WENGINE TAKATAKA.

    ReplyDelete
  3. no no mwakiembe kule kwenu awakupendagi nani aliye kupigia kura wewe acha uzushi wa kutaka uonekane mwema usoni pa watu. umeshinda kwa hila... halafu una sura mbili ya nuruni na ya gizani acha kujipigia debe kiaina sitaki nataka.

    ReplyDelete
  4. Acheni matusi ongeeni mambo ya maana. kuna waziri mwenye jina lenye kutukuka Bungeni kwa ujasiri na ufanisi wa kazi kama jina la Mwakyembe? Yeye amehojiwa na waandishi juu ya uvumi wa mitandaoni kuhusu kutajwa jina lake, ninyi mnaleta matusi wakati yeye amefafanua tu jinsi taratibu zilivyo. by the way what and who is ukawa kumtishia Harrison?Kunyweni maji mpooze miili iliyochemka kwa kushindwa katika uchaguzi mkuu wa Uraisi.

    ReplyDelete
  5. kama uvumi huu wa mwakyembe kuteuliwa waziri mkuu utakua ni wa kweli,basi mimi nitakuwa tayari nimekwisha kata tamaa asilimia mia moja na utawala mpya wa mheshimiwa magufuli.kwa maoni yangu mwakyembe ni mwizi mkubwa na ndiyo maana hapa mwishoni kikwete alimwondoa ujenzi kumpeleka jumuia,na sitta alipopelekwa pale japo ni rafiki yake akatangaza kuukuta ubadhiritu wa kutisha wizarani na kwenye taasisi zake.mwakyembe ni mwizi,ni majanga.mwache apiganie ushindi tata wa ubunge wake mahakamani na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  6. Tabia ya CCM kuchaguwana wagonjwa
    Fyuuuuuuuuuuu
    Magufuli nawe u mzimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
    Au una umeme

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad