Mwanamke Ashambuliwa Kwa Kuzungumza Kiswahili Marekani

Mwanamke aitwaye, Asma Jama ameshambuliwa nchini Marekani kwa kuongea Kiswahili.

Jama alikuwa amekaa na familia yake kwenye mgahawa wa Applebee huko Minnesota, akikata kiu na juice huku mazungumzo yakiendelea kabla ya kujeruhiwa vibaya mdomoni. Mwanamke aliyekuwa amekaa jirani yake alimponda na glasi nzito ya bia mdomoni.

Sababu? Jama alikuwa akizungumza Kiswahili na familia yake.

Siamini baada ya miaka yote hii mtu ananipiga sababu niko tofauti,” alisema Jama. “Mtu ananipiga kwasababu nilikuwa nikizungumza lugha ya kigeni.”

Shambulio lilimwacha Jama na majeraha usoni pamoja na mdomo kuchanika kiasi cha kushonwa nyuzi 17.

Jodie Burchard-Risch, 43, na mume wake, walikuwa wamekaa kwenye mgahawa huo jirani na Jama, aliyekuwa ameketi na binamu na watoto wa nduguze. Wawili hao walichukizwa baada ya kumsikiliza Jama na familia yake wakizungumza lugha ngeni.



Jama alisema wawili hao waliwaambia waende nyumbani. “Walisema ukiwa Marekani unatakiwa kuzungumza Kiingereza.”

Jama, ambaye ni msomali, alihamia Minnesota mwaka 2000 kutoka Kenya. Anazungumza lugha: Kiingereza, Kiswahili na Kisomali.

Jumatatu hii, Burchard-Risch alishikiliwa kwa kosa la shambulio.

Kutokana na shambulio hilo, Jama anadai hana amani tena na anafikiria kuhama Minnesota. Amesema anaweza kuungana na dada yake aliyehama Minnesota mwezi June na kwenda Dallas.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa wazungu hawatupendi na sisi tusiwapende vilevile walitaka wawe pekeyao hapa duniani

    ReplyDelete
  2. Nilidhani anataka kurudi Somalia au Kenya, kumbe bado hataki kuhama ila anazunguka humo humo

    ReplyDelete
  3. wakifika mwenge waongee kiswahili,kama mambo ndio hayo,au bongo ,zanzibar,na nchi zote zinazo ongea kiswahili,kwanza inabidi tuandamani kwa kuwa huo ni ukoloni wa aina yake unataka kurudi duniani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad