Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, amekalia kiti hicho kwa kuanza kuonja 'joto la jiwe' baada ya kushindwa kujibu swali lililomtaka aeleze muda gani aliojiunga na Chama cha Mapinzuduzi (CCM) huku akikumbana na zomea zomea kali kutoka kwa wabunge wa vyama vya upinzani.
Mtafatuku huo uliibuka ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana, wakati Dk. Tulia alipokuwa akijinadi kwa wabunge kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Naibu Spika.
Nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa pia na Mbunge wa Kaliua (Cuf), Magdalena Sakaya, ambaye kura 101 alizopigiwa hazikutosha kumfanya akalie kiti hicho dhidi ya Dk. Tulia aliyepata kura 250.
Hata hivyo, swali lilosababisha bunge hilo kuvurugika lilitoka kwa Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema), ambaye alimtaka Dk. Tulia atoe ufafanuzi muda wa uanachama wake ndani ya chama hicho, na kama mtumishi wa serikali ataje siku aliyotangaza kuachia ngazi na kujiunga na CCM kwani sheria na kanuni za utumishi wa serikali inamzuia kujiunga na chama chochote cha siasa.
“Nakuomba utulieleze sisi wabunge kwa kuwa wewe ulikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa mujibu wa sheria inafahamika wazi kuwa mtumishi wa serikali hasa katika ngazi yako hukutakiwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Tunaomba utuambie lini ulijiunga na CCM, hasa kwa ukizingatia hivi karibuni ulisimamia kesi ya mita 100,” aliuliza Matiko.
Swali hilo lilimfanya Spika Job Ndugaye ambaye alikuwa akiendesha kikao hicho kuwauliza wabunge kama linafaa kujibiwa. Wabunge hasa wa upinzani walijibu kwa sauti kwamba hilo ni swali na linapaswa kujibiwa.
“Mheshimiwa Dk. Tulia haya jibu swali hilo,” Ndugai alimtaka kujibu.
Dk. Tulia wakati akijibu alionekana kutumia muda mwingi kufafanua vifungu vya katiba na sheria vinavyozungumzia zuio hilo, jambo ambalo wabunge wa kambi ya upinzani walionekana kutoridhika nalo.
“Kama ulivyosema mimi ni mwanasheria, katiba nimeisoma, sheria zinazozungumzia utumishi wa umma nimezisoma na kanuni zake nimezisoma…nasema hivi kanuni nimezisoma, sheria nimezisoma,” alisema na kukatishwa na sauti za wabunge zikimtaka kujibu swali.
Kutokana na hali hiyo, Spika Ndugai aliingilia kati kwa kuwaomba wabunge kuacha kumzonga mgombea na vizuri wangemsikiliza kama walivyofanya wakati Sakaya akijinadi.
“Mheshimiwa spika yapo makundi matatu ya watumimishi wanaokatazwa kuwa wanachama na vyama vya siasa, kwanza ni wanajeshi ambao ni polisi na wanao…,” alijibu Dk. Tulia na kukatishwa na zomeazomea kutoka kwa wabunge.
Hata hivyo, Spika Ndugai alisimama na kumuamuru Katibu wa Bunge kuendelea na taratibu za uchaguzi.
Baada ya uchaguzi, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, alimtangaza Dk. Tulia mshindi baada ya kupata kura 250 sawa na asilimia 71.2 wakati Sakaya akipata kuta 101 ambazo ni sawa na asilimia 28.8 za kura zote.
Alisema wabunge wote waliosajiliwa walikuwa 369, lakini idadi ya waliopiga kura ni 351.
Kutokana na matokeo hayo, Spika Ndugai alimtangaza Dk. Tulia kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo na kumuapisha rasmi kuanza kazi yake hiyo mpya.
Naibu Spika Wa Bunge, Tulia Ackson Mwansasu Jana Alizomewa na Wabunge wa UKAWA Baada Ya Kushindwa Kujibu Swali
10
November 20, 2015
Tags
Acha unafiki wewe uliyeleta hii mada kwani hao Ukawa walipanga kuzomea kwa kila jambo litakalofanywa na ccm pale bungeni,mimi nipo hapa bungeni na najionea kila kitu kinavyoenda.Mwana ccm akitaka kuongea wao ukawa kwa utoto wao wanazomea ili asiweze kufikisha ujumbe na ndivyo walivyojipanga leo wamzomee mh.Rais lakini sijuhi kitakachotokea!
ReplyDeleteHAKUSHINDWA KUJIBU, ILA HAO CHADEMA HAWAKUMPA MUDA WA KUJIBU, KILA ALIPOTAKA KUJIBU WANAMZOGOMA KWA MANENO MAKALI, MAKELELE, FUJO KAMA WATOTO WADOGO .........POLE YAO WALOWAPA KURA HAO WABUNGE..........HAPA KAZI TU
ReplyDeleteUKAWA HAMNAZO KWELI,KWA NAMNA MNAVYOZUA UJINGA KILA ITWAYO LEO HAMJUI KAMA MNAMPA MTAJI ZITTO NA ACT YAKE?SIKUPIGA KURA LAKINI WALIOCHAGUA CCM HAWAKUKOSEA.
ReplyDeleteKikwapa hiki
ReplyDeleteAlipanic jamani
ReplyDeletePole unajuwa amebebwa si mataschi yake jamani tumpe subira hakutegemea nafasi hii
Lowasa na Juma Duni wao muda wao wa uana chama ulikua vipiii,,,,Ester Bulayaaaa tetea wana nchi wa jimbo lako sio kuleta zomezomea Bungeni.
ReplyDeleteAngalieni umri wake alivyobebwa hata ungekuwa wewe ungepanic
ReplyDeleteBunge si mchezo
LILIKUWA SUALI LA MHE.HOMBE.YAANI MAJIBU MAJANGA,AIBU,UWEZO MDOGO,MCHECHETO.HIVI KWELI CCM KAZI YA UNAIBU SPIKA ILIKOSA MBUNGE MZOEFU WA CCM ALIYERUDI BUNGENI KWA KUCHAGULIWA BAINA YENU NYINYI 258 MPAKA HUYU AKAACHISHWA KAZI YAKE,AKATEULIWA MBUNGE WA UTEUZI NAMBA MOJA HARAKA-HARAKA ,CCM WAKASAHAU KUMPA KADI YA UANACHAMA.JANA AMETESEKA,AIBU,ALIOGOPA KUJIBU UONGO NI ADHABU.HATUFAI HATA KWA MAJARIBIO,HALIJUI BUNGE,MBUMBUMBU.
ReplyDeletehafai uwezo mdogo.yeye magufuli angempa ubunge wa uteuzi abaki mbunge wa kawaida. nina imani angetoa mchango mzuri kama mbunge wakati huo huo akilizoea bunge kwa kujifunza.hatimaye baada ya miaka 2-3 basi dhamira ingetekelezwa.KWEUPE HAMNA KITU.EWE MUUMBA, TUNAKUOMBA BABA, TUFIKISHE 2020 SALAMA.
ReplyDeleteCCM kubebana kwa sababu mdogo na elimu lazima afuate masharti ya kamati kuu ya CCM
ReplyDeleteChezea CCM wewe