Nuh Mziwanda Adai Aliambiwa ili Asaidiwe Kimuziki Inabidi Asafirishe Unga

Baada ya Shilole kudai kuwahi kushawishiwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya katika muziki wake, mpenzi wake Nuh na yeye amekiri kukutana na changamoto hiyo hiyo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Nuh alisema kama angekuwa anataka mafanikio ya haraka angekuwa ameshapotea.

Wengi waliokuja walikuwa wananiambia issue za kuuza madawa ya kulevya, nianze kusafiri ili niweze kupata pesa ya kuendeleza muziki wangu,” alisema Nuh.

Aliongeza, “Mimi ni mwanaume niliyekamilika na nilichagua kuishi katika maisha yangu, sikuchagua maisha ya kuuza madawa ya kulevya, nimechagua maisha ya kuishi mimi ni mwanamuziki na kupata pesa kupitia muziki wangu. Kwahiyo maisha pia ni chaguo lako wewe mwenyewe ambaye unaishi. Kama umechagua kuishi maisha yako kwa shortcut utapata vitu kwa shortcut na maisha yako yatakuwa shortcut vile vile.”

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waongo hawa wangefuatwa Na Ridhiwani
    Wangeketaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  2. Apo nakuaminia mtu wangu ongeza Bidi ipo siku ..... Utakuwa juuuu👍👍👍

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad