Rais Jakaya Kikwete Atangaza Kuwa Kesho ni Siku ya Mapumziko Tanzania..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.

Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

4 Novemba, 2015

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtuletee Na mabasi Kama kwenye kampeni mtaanu mtubebe

    ReplyDelete
  2. kwanini isiwe siku ya jumamosi
    Au tayari fundi kasema Alhamisi,
    Tanzania nchi masikini watu wafanye kazi , mitihani nk
    Watoa misaada inatuuma sana
    Kumbukeni hata ulaya tuna shida tunao wakimbizi kibao na ni ndugu zetu na jirani zetu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad