Rais John Magufuli, Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Wanakusubiri Uwasaidie Kwa Hili

Nachukua nafasi hii kwanza kumpongeza Rais mpya wa Tanzania Mh. John P. J.Magufuli aliyeapishwa hivi leo. Namtakia kazi njema na kila la heri katika kutimiza majukumu na ahadi zake.

Pili,nawasilisha jambo la muda huu tulionao linalohitaji ufumbuzi wa haraka wa kiserikali. Imesharipotiwa kuwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wamekosa mikopo. Wanaelekea kukwama kupata elimu yao ya juu kwakuwa wengi wao wanatokea familia za kipato cha chini.

Mh. Rais Magufuli,wanafunzi wa vyuo vikuu wana imani kubwa nawe na Serikali utakayoiunda. Wanakusubiri uwasaidie kutatua matatizo yao ya mikopo kama ulivyoahidi ulipokuwa ukipiga kampeni zako. Hakika,wanafunzi wa vyuo vikuu,hasa wale wa mwaka wa kwanza,wanahitaji suluhisho la mikopo yao ya elimu ya juu haraka iwezekanavyo.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acheni yawakute CCM hiyo
    Wametumia 1000000000000000000000000000000000000000000000
    Kwa kampeni ndo maana magufuli mguu WA kwanza fedha hakuna kitu
    Mtajuta kuchagua CCM
    Magufuli si mbaya ila chama chake poleni

    ReplyDelete
  2. Mamvi aliwaambia mchagueni ili msome chuo kikuu bure mkamwona hafai isipokuwa chama cha mafisadi(CCM), na bad, kweli namba mtaisoma kama walivyowaimbia.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad