Rais Magufuli akabidhiwa rasmi ofisi Ikulu na Rais Mstaafu Kikwete

MAKABIDHIANO YA TAARIFA RASMI IKULU.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amepokea taarifa rasmi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo mchana na kushuhudiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Maafisa wa Ofisi Binafsi ya Rais.

Utaratibu wa kukabidhiana Ofisi katika Ofisi Kuu hapa nchini ni jambo la kawaida na hivyo imebidi makabidhiano hayo kati ya Rais anayeondoka na anaye ingia madarakani kufanyika.

“Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi” . Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne amemueleza Mhe. Rais Magufuli wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.

Mhe. Rais Mstaafu amekabidhi taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile ambazo zinasubiri maamuzi ya utekelezaji. Mengine ni hali halisi ya nchi katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa muongozo wake siku zote .“Nikushukuru kwa kuiacha nchi salama na itaendelea kuwa salama, nikushukuru kwa muongozo wako, na taarifa ya muelekeo na ninaahidi kuwa Hapa ni Kazi Tu”.
 
Mhe. Rais amesema na kumueleza Rais Mstaafu kuwa ametengeneza mazingira mazuri ambayo nchi nyingi zimeshindwa kufanya na hivyo basi kuahidi kuendelea kuchota hekima na busara kwa Marais wote wastaafu wakiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa wa Awamu ya Tatu na Mzee Ally Hassan Mwinyi wa Awamu ya pili.

Wakati huo huo Mhe. Rais Magufuli ameendelea kupokea salamu za pongezi kutoka Kwa Msimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bibi Helen Clark.

“Chini ya uongozi wako, tunatarajia kuzidi kuimarisha ushirikiano baina yetu, demokrasia, kushughulikia masuala ya umaskini na ajira kwa vijana , kukuza uchumi, na kulinda na kuhifadhi mazingira, masuala ambayo Tanzania na UNDP tumekuwatukishirikiana kuyaendeleza na kuyatimiza” amesema Bi Clark.

Salamu zingine ni kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Uswiss, Mhe. Simonetta Sommaruga, Rais wa Jamhuri ya Italia Mhe. Sergio Mattarella, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Joachim Gauck na pia kutoka kwa Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.

Pongezi zingine zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya Urusi, Mhe. Vladimir Putin, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Park Geun-hye na kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. XI Jinping.

Salamu pia zimemfikia Mhe. Rais Dkt. Magufuli kutoka kwa Rais wa Taifa la Eritrea Mhe. Isaias Afwerki na kutoka kwa Rais wa Ufaransa Mhe. Francois Hollande.Katika ujumbe wao, viongozi hao mbali na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamesisitiza kuendeleza na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao.

Pia wameipongeza Tanzania kwa kudumisha demokrasia imara na Watanzania kwa ujumla kwa kuimarisha amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Novemba, 2015

Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati akiongea kabla ya kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015

Rais Dkt John Pombe Magufuli akipokea kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiiangalia kwa furaha hati ya makabadhiano ya Ofisi aliyoipokea kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015
Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makiamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya hafla ya makabidhiano rasmi ya Ofisi Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi leo Novemba 12, 2015.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haijarishi toka mwana kwenda
    Umeicha nchi nyeupe kwa u vasco dagama wako
    Zanzibar Na majizi yote yanatesa wengine ni wabunge WA CCM
    Shame you kikwete

    ReplyDelete
  2. Magufuli fukuza huyu kibanga mtoto mshenzi sana huyu asikuchaguliye watu
    Salma hampendi pamoja na kuwa JKT Ruvu

    ReplyDelete
  3. Hakukabidhi kabla hajaondoka ccm Acheni sinemaaaaaaaaaaaaaa
    Pesa ngapi serikali inalipia gharama hizi
    Mtu mzima ovyo kikwete Kama unajua ungeanza Na ya Zanzibar kwanza
    Wanzanzibar Na Watanzania tutakulani kwa hili

    ReplyDelete
  4. Salam za uongo hizo toka ulaya na USA

    ReplyDelete
  5. ina-wauma hiyo......
    ina-wachoma kama pasi.......

    Aliyepewa-kapewa........kama unaweza, panda juu kazibe......

    ReplyDelete
  6. Mbona hamjaonyesha nyumba yake ya Msoga
    CCM wiziiiiiiiiiiiiii hekalu la Msoga wachaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  7. Kaletewa uganga bibi
    Lakini
    Wasukuma kiboko yao kaondoka yake kikwete

    ReplyDelete
  8. ANAKUKABIDHI SERIKALI HUKU NYUMA HATUELEWI.JEE KWA SASA DENI LETU LA NJE LIMEFIKIA KIASI GANI? MBONA MMEKAA KIMYA HAMSEMI? PILI MADENI YA NDANI YAKOJE?MTAANZA KUYALIPA LINI?TATU KWA MHE.MAGUFULI YALIKUWEPO MATUMIZI YA UFUJAJI MKUBWA SANA SERIKALINI KUANZIA HAPO IKULU OMBI:MPIGE NYANI,USIMUANGALIE USONI,NA WANANCHI TUSHUHUDIE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad