Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amesema atamfikisha mahakamani Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kuvunja kanuni baada ya kuwaingiza polisi ndani ya ukumbi wa chombo hicho.
Polisi hao waliingia ndani ya ukumbi huo wiki iliyopita wakati Rais John Magufuli alipofika kwa ajili ya kuhutubia Bunge.
Kubenea alisema kitendo cha askari kuingia ndani ya Bunge kwa mara ya mwisho kilitokea nchini Uingereza mwaka 1930 na hakijawahi kutokea tena isipokuwa nchini.
Alisema kuwa kesi hiyo anatarajia kuifungua Mahakama Kuu wiki ijayo kwa ajili ya kutaka tafsiri ya kanuni hiyo.
Hata hivyo, mkurugenzi wa shughuli za Bunge, John Joel alisema hakuna kanuni iliyovunjwa kwa askari hao kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Wakati Kubenea akiandaa mpango huo, Kamati ya Wabunge CUF imesema Spika Ndugai ndiye chanzo cha yaliyotokea bungeni.
Ijumaa wiki iliyopita wakati Rais akiingia kutoa hotuba ya kuzindua Bunge, wabunge hao walipiga kelele wakitaja jina la mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuonyesha msimamo wao dhidi ya uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa visiwa hivyo.
Walipiga kelele hizo wakati Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein akiingia kwenye ukumbi huo na baadaye wakati Dk Magufuli akiingia ukumbini na wakagoma kunyamaza hadi walipotakiwa kutoka nje na askari kuitwa ndani.
Wabunge wa upinzani wanadai kuwa Dk Shein si Rais wa Zanzibar, wala makamu wake wa pili, Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho kwa madai kuwa muda wao uliisha Novemba 2, baada ya Uchaguzi Mkuu.
Jana wabunge wa CUF chini ya Mwenyekiti wake, Juma Hamad Omary walitoa tamko lililokemea na kutoa tahadhari kwa mambo mawili huku wakimtaka Ndugai kutoyumbishwa na Serikali.
Katibu wa Umoja huo, Hamudu Hassan Bobal alisema vurugu zisingetokea endapo Bunge hilo lingezingatia tamko la barua ya Ukawa na kusikilizwa hoja ya mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyeomba mwongozo akitaka kujua Dk Shein na wenzake wanaingiaje bungeni wakati madaraka yao yaliisha tangu Novemba 2.
Hiyo ndio kazi mlobaki nayo Chadema, ni mahakamani, mahakamani, mahakamani...........kwa hiyo mlitaka muachwe mpige kelele kama vichaa, hebu pelekeni mbele viroba na bangi zenu, hamumtishi mtu hapa, sio mahakama kuu ya TZ, nendeni the Hague.........
ReplyDeleteHivi huyu Kubenea si ndio yule alomwagiwa tindikali na Lowasa kipindi kile alipomwandika vibaya.......... sasa hivi nayeye kawa fisadi, wameunda 'ushoga' na FISADI PAPA eti wanaelewana hahahahahaha amakweli 'WASIO NA HAYA, WANA-MJI-WAO'
ReplyDeletePolisi wanaingia na kukulinda mpaka ndani unakolala na mkeo nini bungeni?UKAWA ifikie mahali muheshimu wananchi na sio kila siku ujinga na kesi zisizokuwa na maana
ReplyDeleteKuna ki bi Tulia kitakuja na vijibu mshindoo mtaniambia
ReplyDeleteHuyu kubenea aendelee na mpango wake huo mwisho WA siku ataambulia matokeo ya kesi ya 200 Mita. Darasa la Sana hawezi kushinda kesi.
ReplyDeleteSpika Job Ndugai aidha kwa kuagizwa au kwa kutokana na moyo wake wa kikatili,roho ya kikatili,mawazo ya kuelemewa na shetani,ubabe wa kishamba,kujionyesha anajua kumbe hajui,kwa kitendo chake cha kuandaa squadron ya askari wa jeshs la polisi,kwa kuwakosea heshima wananchi wa Tanzania kupitia kwa wawakilishi wao waliojizolea mamilioni ya kura,weka pembeni wale wezi waliopo bungeni kwa kusimikwa na tarakimu za kupikwa na TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI,waliingia bungeni kuvamia[storming-]kama vile wanakwenda kuwaokoa mateka wa kijeshi.huku wakiwa wame cork silaha zao kama vile ni kuingia na kupambana kijeshi kutumia mtutu wa bunduki.kwa kumvamia mbunge wangu ukiwa umemuelekeza silaha maana yake nini?kwa nini usiingie mikono tupu uniform yako pekee ikuwakilishie ujumbe uliotumwa na ndugai? kwa nini usiingie na kirungu ambacho ni dalili za kawaida za askari wetu kazini,lakini la msingi tunalolilaani na kulikataa kwa nguvu zote NI KWA NINI NDUGAI ALIAMURU POLISI WENYE SILAHA ZA KIVITA WAINGIE BUNGENI KINYUME KABISA CHA UTARATIBU WA MABUNGE DUNIANI KOTE,KWA DHAMIRA YA KUWADHURU WABUNGE WA UKAWA WALIOKUA MIKONO TUPU.MASHTAKA KWA NDUGAI YASAMBAZWE MABUNGE YA DUNIANI KOTE.DUNIA ITUSAIDIE KUTAFSIRI UKANDAMIZAJI HUU NA,KUULAANI KWA NGUVU ZOTE..
ReplyDeletePUNDA HAENDI BILA BAKORA..................WAPIGWE, WATANYOOKA TU
DeleteNYIE WEZI WA KURA,MAJAMBAZI WA SIASA.MAZUZU LETENI TUU KEJELI ZENU ZA KISHAMBA LAKINI MWISHO WA SIKU MACHUNGU TULIYONAYO YATAWAGEUKIA
ReplyDeleteMtasubiri sana...HAPA KAZI TU
DeleteHe he he, ukiingia huku stress zote zinaisha
ReplyDeletekubenea wananchi wako ubungo wanalala nje wewe unahaha na mahakama. tunajutaje kukuchagua naona umeliingia bunge kwa jazba. mbona yatakushinda!! umekuwa mbunge wa mahakama na kelele badala ya wananchi wa ubungo. tunajutajee????
ReplyDeleteHahaaaaaa ni shida..ama kweli ukiingia huku unatoka huna stress.
ReplyDelete