Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Club, Steve Nyerere amesema aliulizwa kwa zaidi ya mara sita na Rais Dk John Magufuli kuhusu nsaada wanaouhitaji, lakini amedai alishindwa kumjibu kutokana na wasanii wengi kutojitambua.
Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV, Steve alisema alimwambia Magufuli asipoteze pesa ya serikali kuwasaidia wasanii wa filamu.
“Sikatai,” alisema Steve. “Nilishamwambia mheshimiwa rais, utapoteza pesa zako, nilisha mwambia mstaafu na huyu mpya utapoteza pesa!
Kwa sababu lazima tukae chini tujitafakari tunataka nini? Mimi ni mtu niliyewahi kuulizwa na mheshimiwa Magufuli zaidi ya mara 6, niliulizwa na mheshimiwa rais tukiwa Morogoro. Serikali haiwezi bila sisi wenyewe kujitambua hata uweke mabilioni ya pesa,” alisisitiza.
Pia Steve alisema wasanii wengi wamejivisha joho la usanii wa filamu lakini hawafanya kazi.
“Kwanza tuna asilimia 90% ya watu kwenye hii industry ya filamu hawajaingia kufanya kazi,” alisema. “Ukichunguza sana watu wamekuja kuuza sura, ukichunguza sana asilimia 90% walioingia kwenye filamu, 6 au 5 ndio wana nia ya kufanya kazi. Hawa wote walioingia wanaingia wapate jina wafanye mambo yao ambayo sio ya kuinua sanaa.”
Kwenye mahojiano hayo pia Steve alisema tasnia ya filamu nchini imefika sehemu mbaya na inaelekea kufa kabisa.
Steve Nyerere: Nilimwambia Rais Magufuli Kuwasaidia Wasanii wa Bongo Movies ni Kupoteza Pesa..Wengi ni Wauza Sura Tuuu
3
November 20, 2015
well said Steve
ReplyDeletemtoto mbuzi,hana mpango wwt,anaumbuka sasa.mwanao akiunyea mkono utaukata au mtengenezee mazingira thabiti??,ikiwemo shule za usanii,sanaa. certificate,deploma hadi degree.mastudio ya ukweli,wahindi hawali jasho la msanii.wasanii walipe tax nk..we unakurupuka tu husiwasaidie unataka usaidiwe wewe tu..huna mpango wwt wewe..
ReplyDeleteohoo nataka udc...kwa elimu gani uliyonayo..kimtazamo tu anaonekana ni kana roho mbaya...
ReplyDelete