Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia.
Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.
Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari za upotishaji.
“Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa,” amesema Mwambene.
Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.
“Mkapa yupo hai na kesho pia atakuwepo katika sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” amesema Mwmbene na kuongeza.
Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi ya watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma kupotoka.
Amesema kuwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi wao iwe ya usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi zao.
Taarifa ya Serekali Kuhusu Taarifa za Kifo cha Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa Zilizozagaa Mitandaoni
3
November 04, 2015
Tags
Kama kawaida yao CCM
ReplyDeleteKuficha magonjwa hadi vifo kisa shughuli ya kesho
Kama hajafa kesho awepo kwenye kuapishwa basi
Hilo limewagusa, ila la kunadi fulani MGONJWA MLILIONA ZURI SIYO?!! Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu,
ReplyDeleteYaani huyu Kipipa na Tezi Dume wakikauka leo, itakuwa ni furaha ya Taifa zima!!.. Huyo mteule wa NEC yupo tu hapo kama kin`gamuzi.
ReplyDelete