TB Joshua Ayeyuka Ghafla...... Aacha Maswali Mazito Hapa Nchini

Muhubiri wa kimataifa nabii maarufu duniani Temipote Balogun maarufu kama TB  Joshua ameacha maswali baada ya kushindwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa awamu ya tano Dk.John Magufuli.

TB Joshua aliwasili nchini November 03 kwa ndege binafsi na kupokewa na Dk.MAGUFULI pamoja na Mbunge mteule Mwigulu Nchemba katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere,Dar es salaam.

Baada ya kuwasili alifanya mazungumzo ya faragha na Dk.MAGUFULI pamoja na rais mstaafu Jakaya Kikwete kisha kufanya mazungumzo zaidi ya saa tatu na Edward Lowassa.

Ujio wa nabii huyo ulionekana kama amekuja kwa ajili ya kuapishwa kwa Dk.Magufuli lakini huku baadhi ya wananchi wakifurahishwa na ujio wake na kuamini ni fursa pekee ya kukutana naye na kufanya maombi akiwa hapa nchini.

Baadhi ya watu walisema waliamua kwenda uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kumuona nabii huyo lakini haikuwa hivyo na hawakufahamu kwa nini hakuhudhuria sherehe hizo
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UMPIGE CHANGA LA MACHO NABII MAARUFU NA MHUBIRI MAARUFU DUNIANI NABII J.B.JOSHUA,THUBUTU!.ALIKUJA,TENA KWA KUALIKWA,AKAONA,AKAZUNGUMZIWA,AKAOGOPA,AKASHANGAA,AKAPANDA NDEGE KUREJEA ALIKOTOKA HUKU ANATUSIKITIKIA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  2. Na nyinyi wabongo mlivyokuwa ubwete kuibiwa basi ah hawa manibii , ma mufti na akina maalim fake wanawaibia tu kudadeki toeni matongotongo machoni mnakera sana mwadamu katika maisha yake ya kila siku kuna kupata na kukosa kuna kuugua na kadhalika coz that's how life's all about and no one can under the sun change it so stop that bullshit old fashion way of thinking ya kuabudu binadamu mwenzio

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad