TB Joshua ni Mgeni wa Nani Nchini Tanzania? Maswali Yazidi Baada ya Kutoonekana Uwanja wa Taifa Katika Sherehe za Kuapishwa

Kinyume na ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari Hajaonekana kwenye sherehe za kupishwa kwa Mh. Rais na wala jina Lake halikuwemo kwenye orodha ya wageni.

Hivi majuzi muhubiri maarufu kutoka nchini Nigeria TB Joshua aliwasili nchini kwa kile kilichoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo gazeti la Mwananchi kwamba muhubiri huyo amekuja nchini kushuhudia kupishwa kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli.

Alipowasili uwanja wa ndege hapa Tanzania alipokelewa na baadhi ya viongozi walioongozwa na Dr. John Pombe Magufuli na akaenda moja kwa moja kumsalimia Rais Kikwete Ikulu magogoni Dar es Salaam.

Baada ya kutoka Ikulu muhubiri huyo alielekea nyumbani kwa aliyekuwa mgombea urais wa UKAWA na waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa eneo ambalo ameonekana kuwepo kwa Muda mrefu akizungumza na Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA.

MASWALI

1. Je, ujio wa Muhubiri huyo ilikuwa ni msafara binafsi Kinyume na ilivyoripotiwa na vyombo vya habari?

2. Vyombo vyetu vya habari havikupewa taarifa sahihi kuhusu sababu za ujio wa kiongozi huyo?

3. Kama ni msafara binafsi kwanini apokelewe na rais mteule na kutembelea Ikulu?

4. Je ni viongozi wa UKAWA wamemzuwia kuhudhuria sherehe hizo za kupishwa Rais kutokana na wao kugomea kusaini matokeo?

5. Je, bado yupo nchini? Maana kama tulijulishwa kuhusu ujio wake si vibaya tukajuzwa kuhusu kuondoka kwake.

Nawasilisha:
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aliyekwenda kumpokea ndie alikuwa mwenyeji wake,na hakuhudhuria uwanjani kwa sababu binafsi( hutakiwi kuzijua).alikwenda ikulu baada ya kuomba akamsalimie mh.kikwete,alikwenda kwa Lowasa baada ya Lowasa kuomba anaomba kuonana nae,
    Wewe wapi ulitangaziwa kwamba Tb Joshua anakuja TZ kama sio kustukizwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtaficha mengi lakini siku yatatoka tu

      Delete
  2. UWE NA UHAKIKA NA HABARI KABLA YA KUANDIKA.KAENDA KWA MAGUFULI,KAENDA IKULU,KAENDA KWA LOWASA.KILA MAHALI KAACHA UJUMBE,NA HAWEZI KUZUIWA NA MTU KUFANYA JAMBO YEYE HUSIKILIZA ROHONI MWAKE ANATUMWA NINI.UJUMBE KWA KIKWETE TULIUSIKIA KWAMBA NI PONGEZI NA KUCHAGUA RAIS WA BARAKA NA FANAKA KWA HURU NA HAKI,UJUMBE UPANDE WA PILI HATUJUI MAANA HAWAJAWA WAZI.LAKINI NAAMINI NI MADONGO MAANA JOSHUA HUWAGA HAKOSHI PENYE KASORO HATA KWA MKE NA MUME.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Alisema kikwete mwenyewe au Joshua

      Delete
  3. Hamuwezi fahamishwa kwani mnakurupuka tu bila kujua chochote. Unajua Lowassa anahitaji kuombewa laa sivyo anaweza pata maradhi ya moyo ao tatizo la saikolojia hivyo ikulu ilimuitisha ili aje kumuombea na kuepukana na hizo tatizo nilizozitaja hapa. waandishi wengi wameonesha udhaifu wao wakati wa kampeni na ndiomaana hawatakua wanashirikishwa ao kufahamishwa na taarifa mbali mbali. Mwandish wa habari haangalii faida zake binafsi bali zakazi na kujitambua kwamba yeye anatumikia taifa na dunia kwa ujumla sio ushabiki kutokana na faida zake binafsi no no no neverrrrrr.

    ReplyDelete
  4. Ukishapata majibu ya hayo ya maswali yote tapata faida gani?? Fanya kazi ujenge taifa lako, wacha uzembe

    ReplyDelete
  5. ALIKATAA KUHUDHURIA SHEREHE,AKAONDOKA.SIMAMA HAPO HAPO,ALIKATAA.

    ReplyDelete
  6. kwani akuapishwa au kaapishwa?kaapishwa na maisha yanaendelea kama kawaida.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad