Ubovu wa Fifaa Hospitali ya Muhimbili..Mtaalamu Aongea Kuhusu Sakata Zima na Nani Anapashwa Kuwajibika

Ukweli usemwe na wakuwajibika na kuwajibishwa na wawajibike kwa haki!

Niseme tu sipingi na kamwe sitapinga kasi ya Magufuli katika kufanya maamuzi...maamuzi yote magumu lazima yawe na setbacks na regrets lakini yanaheshimika kuwa ni maamuzi magumu.

Kiongozi ni yule anayechukua maamuzi hata kama atakosea au kuumiza wengi.

Hii ndio kasi inayohitajika kwenye mfumo mbovu unaoficha maovu yake chini ya mwamvuli wa 'utaratibu'

Ubovu wa CT SCANNER NA MRI Muhimbili ni rflection ya tatizo kubwa na la msingi katika hospitali nyingi au zote nchini.

Kwa uelewa wangu hadi jana ni kwamba wizara ya afya iliingia mkataba na kampuni flani (sitaitaja jina) kufanya matengenezo ya vifaa tiba aina ya CT scan na X rays na Ultra sounds na vinginevyo.

mkataba huu ulifanyikia huko huko wizarani.

Mojawapo ya kipengele cha mkataba ni kwamba vifaa hivi haviruhusiwi kutengenezwa na mwingine yoyote zaidi ya yule aliyepewa tenda huko wizarani.

Yoyote au taasisi yoyote itakayokiuka kipengele hiko kwa kutengeneza vifaa hivyo na kwa bahati mbaya vikafa kabisa basi itakuwa imekula kwake.

Kipengele hiki kinaweza kuwa sababu ya uongozi wa MNH au hospitali nyingi kutozigusa vifaa hivi kwa matengenezo ya kawaida au dharura.

Tetesi zilizopo ni kuwa malipo ya huyu mzabuni hayakwenda sawa kwa muda mrefu kwa hiyo walivisusa au kuvitekekeza vifaa hivi .

Kwa hiyo kwa mkurugenzi anayeamini katika 'taratibu' angeweza kuendelea kusubiri wizara na mzabuni wamalizane ili mashine hizo zije kutengenezwa.

Ni common practise kuwa viongozi wa mahospitali wakijaribu kuwasilisha tatizo hili wizarani au kwa mzabuni kupewa majibu ya tunashughulikia...

KOSA LA DIRECTOR WA MNH!

Kama kiongozi wa 'zahanati' kuu alitakiwa kulichukulia tatizo la CT SCAN NA MRI kutokufanya kazi kuwa ni tatizo kuu na la kutisha na linalohitaji special attention

Alitakiwa kutokulala,kuumizwa na kulihangaikia toka siku ya kwanza.

Alotakiwa kulipresent kwa wadau wote ikibidi hata kulifikisha Ikulu na kulielezea umuhimu wake kama ukosefu wa umeme nchini.sidhani kama alifanya enough katika hili...pia sidhani kama wakuu wengi wa hospitali nyingi za serikali wana hulka hii ya kuyaelezea matatizo ya hospitali zao.
Hilo ndilo kosa pekee kama hukumu yake ilibase katika ukosefu wa huduma za ct scan na MRI!!

WANAOTAKIWA KUWAJIBISHWA KWENYE SAKATA HILI...ukiacha ditector wa MNH!

Kama nilivyoekeza hapo juu...mkataba huu wa maintanance uliingiwa juu kwa juu huko huko wizarani.

Kwa hiyo wapo wengi tu ambao wanaotakiwa kuwajibishwa...

Kuna Director wa Diagnostics yaani anayehusika na mambo ya vipimo hospitalini.

Kuna watu wa procurement aka wazee wa michakato na 10%...

Kuna watu wa hazina waliopeleka B3 jana na sio miezi miwili iliyopita.

Kuna wahasibu wa Muhimbili nikiamini kuwa kuna makusanyo ya fedha za kuweza kutengeneza hiyo mashine.

Kuna maafisa wa procurement hapo muhimbili na wizarani ambao mara nyingi hawajui umuhimu wa vifaa hivi kufanya kazi.

Kuna bodi ya Muhimbili kwa bahati nzuri ilikuwa imemaliza muda wake.

Wako watumishi wengine wadogo wadogo ambao sitawataja.

WAY FOWARD NI NINI?

Bado nakubali hii nginjanginja ya Magufuli ili watumishi wa umma waamke!

Viongozi waliopewa dhamana waelewe kuwa hakuna tatizo dogo au kubwa au la mazoea.

Sheria za manunuzi zilizopo zipitiwe na kuenenda kulingana na sekta mbalimbali...kuna sekta zilizo na uharaka au dharura kwa muda wote.

Rais awawajibishe watendaji wa wizara sio wa taasisi pekee.

Wanasiasa na bodi mbalimbali zifanye kazi kutikana na ushauri wa wataalamu.

Maamuzi mbalimbali yatoke kwa wataalamu walioko 'site' na sio wapigaji wa wizarani.

Wananchi waendelee kupigia kelele huduma mbovu sio tu kwa kuilenga taasisi bali hata executives kwa maana ya wizara.

MWISHO:

Tumekubaliana na Slogan ya #HAPAKAZITU basi tukubaliane kuumizana sana tu mpaka pake tutakapokaa sawa kama taifa.

WASALAAM...HII SIO SIASA NI USHAURI WA #HAPAKAZITU
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Apige chino baraza la mawaziri WA kikwete, what about waziri WA afya na katibu mkuu wake? Corrupted government ya kikwete, watalaanika wote kwa kuwatesa watanzania, shame on you woteee, magufuli safisha kabisa we r so damn tired

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fukuza wote wote
      Ukatibu mkuu si ufalme wote wizi hao

      Delete
  2. mzee wa hapa kazi tu naamini sasa hivi na wewe ni mmoja kati ya wasomaji wa mitandao ya kijamii naungana na mchangiaji wa kwanza usiruhu mawaziri wa kikwete kufanya nao kazi watakuharibia kazi piga chini wote anza upya wapo vijana wengine wenyewe uchungu na nchi yao watafanya kazi siyo hivyo vizee vingine hadi meno yameishia wapo tu wizara isiyo maalum shame on you

    ReplyDelete
  3. Tumepata pakuanzia, mwanzo mzuri

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad