UKAWA Kumpokea Rais Magufuli Bungeni Kwa Staili Mpya

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema utakuja na stahili mpya wakati  Rais Dk. John Magufuli, atakapokwenda  kuzindua na kuhutubia Bunge Novemba 20, mwaka huu.

Umesema staili watakayoitumia ni tofauti na ile waliyoitumia wakati Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, alipozindua Bunge la 10 mwaka 2010 ya kutoka nje ya ukumbi kuonyesha kutotambua serikali yake.

Akizungumza na mtandao huu katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, aliyekuwa Mnadhimu wa Bunge la 10 Kambi la Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, alisema safari hii hawatatoka nje ya ukumbi wa Bunge  hata kama hawamkubali Rais Magufuli, kwa kuwa ni wajibu wao kushiriki vikao vya chombo hicho cha kuwakilisha wananchi.

“Sisi ni wabunge, tumo humu kwa ridhaa ya wananchi, tuna haki ya kuingia bungeni, hivyo siku hiyo tutaingia lakini kitakachotokea tutajua siku hiyo, bali haitakuwa kama walivyotuzoea tunatoka nje,” alisema na kuongeza:

“Subira yavuta heri, bado siku tatu tu, Watanzania watajua msimamo wetu tukiwa ndani ya Bunge,” alisema.

Hivi karibuni aliyekuwa mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa, alisema hawatambui matokeo yaliyotangazwa na Tume yaTaifa ya Uchaguzi (Nec) na kumpa ushindi Rais Magufuli na kwamba hawatashirikiana na serikali yake kutokana na kile alichoeleza kuwa uchaguzi mkuu uligubikwa na wizi wa kura na kuporwa ushindi.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UKAWA MNAJISUMBUA TU NINYI NDIO WIZI WAKUBWA MAFASIDI WA SERIKALI

    ReplyDelete
  2. Ukawa hawana jipya watuache na magufuli wetu waende zao huko

    ReplyDelete
  3. Hapa Kazi Tu!!!!

    ReplyDelete
  4. hivi hawa watu wangepewa nchi so ingekuwa vurugu kila siku nyie ukawa acheni movie zenu kudanganya wa tz

    ReplyDelete
  5. ENDELEENI TU KUTOKA NA MWAKA HUU MTAKIONA NDIO MAANA MNAANZA KUSEMA HATUTATOKA KWA KUWA MNAJUA KITATOKEA NINI NA MWENZENU ALISHASEMA WAKATI WA KAMPENI. TOKENI SASA NJE YA BUNGE.

    ReplyDelete
  6. WATU WAZIMA HAWATISHIWI "NYAU" ANONY 8:38AM. JIFUNZE SHERIA UJUE HAKI NA MIPAKA YA KILA MWENYE MAMLAKA UTAJUA KUWA UNATESWA NA KAMPENI WAKATI ZISHAISHA!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad