UKAWA Wapigwa Mkwara Mzito..Watahadharishwa Wakifanya Vurugu leo Wakati Rais Anahotubia Wataikiona cha Moto

Nape Nnauye
Wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa wameonywa kutofanya jambo lolote litakaloashiria kuvuruga Bunge wakati Rais John Magufuli atakapolihutubia leo jioni.

Akiongea jana mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye alisema kuwa Wabunge hao wa Ukawa wanapaswa kufahamu kuwa kitendo chochote watakachofanya kwa lengo la kuvuruga hotuba hiyo ni kinyume cha sheria na taratibu za Bunge na kwamba hawatavumiliwa.

Nape alionesha kuwashangaa wabunge hao kudai kuwa hawamtambui Rais Magufuli ili hali wanashiriki katika shughuli zote za Bunge ikiwa ni pamoja na kumpigia kura Waziri Mkuu ambaye ameteuliwa na Rais huyohuyo wanaedai hawamtambui.

Naye Mbunge wa jimbo la Nzega, Dkt Khamis Kigwangala alisema kuwa wabunge wa Ukawa wana haki ya kuingia Bungeni na kukaa kwa utulivu au kutoka nje endapo hawatakuwa tayari kusikiliza hotuba hiyo lakini sio kuvuruga hali ya amani ili watanzania wasipate nafasi ya kumsikiliza Rais.

“Hawawezi kuwanyima haki watanzania kumsikiliza Rais wetu akiwa anatoa dira ya uelekeo wa Taifa letu,” alisema Khamis Kingwangala.

Wabunge wa Ukawa juzi walifanya mkutano na vyombo vya habari na kueleza kuwa hawatakubali kumuona Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein akiingia katika Bunge hilo leo kwa kuwa kipindi chake cha urais Zanzibar kimekwisha.
 
Walisisisitiza kuwa watafanya ‘jambo’ ambalo hata hivyo hawakulitaja. Wabunge hao pia walisema kuwa wamemuandikiabarua Spika wa Bunge kuhoji uhalali wa hotuba ya Rais wakati Zanzibar bado haijampata Rais mpya.
Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Lofa ameshakuwa msemaji wa bunge? jamaa mwisho wake mbaya sanaa

    ReplyDelete
  2. Haoohapo eti wanatak kuongoz inchi vipi utaongoz inchi wakat we mwenyew huelew ? et hatumkubal rais kwel kwa mtu alie hetim shul na mweny shahad mbali mbal hawez akasem hayo. Unamkubal spik, jin lilio tolewa na rais kua wazir mkuu na unachagua badaae eti hatumtambui kwel haya yanaingia akilini? achen kuchez akili za watanzania na hoj zenu hazin tija yoyot. Kam hamutak kutumikia watanzania kwa nini uitwe mbunge? vizur jiuzul na pachagulie yul anae taka kutumikia wanainchi sio nyiny weny kulet vurug na ghasia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndugu mbona hata kuandika sawasawa hujui? ndiyo shule zenu za siku hizi zinawafundisha kuandika kijinga hivi? au ni kichwa chako tu, kibovu?

      Delete
  3. WATAKACHOKITEKELEZA BUNGENI UKAWA NI KILE AMBACHO WANANCHI TULIOIBIWA KURA ZETU NA CCM OCTOBA 25 TUMEWAAMBIA WAKIFANYE.HATUNA URAFIKI NA MWIZI KWA MIAKA MITANO YOTE ITAKAYOKUJA.TUTAPAZA SAUTI ZETU "WEZI HAO,WEZI HAO,WEZI HAO" KWA MIAKA YOTE MITANO IJAYO.NGUVU YA UKAWA NI NGUVU YA WATANZANIA WALIO WENGI.WE WILL BE AGAINST EVERYTHING PROVIDED IT IS BEING TABLED BY AN AGENT OF OUR THIEF-THE ARCH ENEMY OF THE PEOPLE.FOR NOW AND,FOREVER.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata mwehu ana namna yake ya kufanya kwa binadamu mwenye akili timamu ili mradi tu aonekane hana mapungufu.Na mtashindwa kwa sababu Mungu wa mbinguni anajua sio watanzania wote wako upande wa chadema,na kwamba ccm iko kwa watanzania wote.

      Delete
    2. Hebu acha kumuingiza MUNGU kwenye Upambavu sina Chama lakin aliyekwambia ccm ya Watanzania wote nani au kwa sababu we una milo mitatu unaish vizur that y you talking pumba ingekua ya Watanzania eote wengine wangekua hawajui hata wanakula nn kwa siku wakati wengine wamelimbikiza pesa hazna matumizi zaidi ya starehe na uhuni acha kumtania Mungu

      Delete
  4. UKAWA,hivi kweli mnawapenda watanzania?mbona kila siku mnatuweka matumbo joto jamani,mbona kila siku mnachochea mambo yasiyo halali kwa wananchi?Yaani ni bora tubaki na umasikini kuliko kumwaga damu,tunaowaomba sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe Anonymous at 10:44 AM,Kumwaga damu kivipi?ebu fafanua

      Delete
  5. Mtu mwenye akili hamskilizi nape hata siku moja

    ReplyDelete
  6. hivi sijaelewa kauli ya kusema wameibiwa kura msidanganye watanzania kama.mmekula oesa za watu kwa ajili ya kampeni lipeni tu ni upuuzi na ujinga mtu msomi eti unasema utafanya fujo hizo ni akili za watoto wa chekechekea

    ReplyDelete
  7. Mbowe na wenzake wote walokula pesa ya Lowasa, wanajitahidi kumzuga na kumwonyesha Lowasa kwamba eti wanampigania haki yake, hebu mrudishieni pesa yake akachunge ng'ombe kama alivyosema mwenyewe, mnampotezea muda tu huku mkijua hilo mtakalo HALIWEZEKANI.......mkajifanya kumpa mkewe ubunge wa viti maalum kupoteza lengo......HEBU MPENI CHAKE BABU WA WATU

    ReplyDelete
  8. HAKUNA MWAKA WALOKUBALI KUSHINDWA, MIAKA YOTE WANAIBIWA WAO TU NA KUSUSIA BUNGE NDIO ZAO, TUMESHAWAZOEA.........HAKUNA JIPYA

    ReplyDelete
  9. UKAWA NI TAMAA YA PESA MAFASIDI KAMA HAWAMTAMBUI MAGUFULI WAMEKWENDA

    BUNGENI KUFANYA NINI KAMA SIO NJAA WAPUMBAVU HAWA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad