UKAWA Wasimulia Kilichowafanya Walete Vurugu Na Kumzomea Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umesema mipango yao ya kutomruhusu Rais Dk. John Magufuli kulihutubia Bunge akiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, imefanikiwa.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Freeman Mbowe, alisema  jana kuwa walimua kuzuia Rais Magufuli asihutubie Bunge kwa vile Dk. Shein, muda wake wa kuwa rais ulikwisha tangu Novemba 2 mwaka huu kwa hiyo hakustahili kuhudhuria Bunge hilo.

Alisema kuwa waliamua kufanya vile wakiamini kuwa ilikuwa sehemu muafaka ya kufikisha kilio chao kutokana na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano ule, wakitokea katika nchi za jumuiya ya kimataifa.

“Tulishangaa kumuona Dk. Shein, Pandu Amiri Kificho na Makamu wa Pili wa Rais wakiwa ndani ya Bunge wakati kikatiba hawana uhalali,” alisema Mbowe.

Alisema, baada ya kitendo kile hivi sasa umoja wa vyama hivyo, unatarajia kukutana ili kupeana mikakati ya kuendeleza mapambano ya ndani na nje ya nchi ya kudai haki.

“Uchaguzi wa Zanzibar hauwezi kutenganishwa kikatiba au kisiasa na uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya muungano,” alisema Mbowe.

Mbowe alisema Ukawa hawako tayari kuinajisi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuruhusu viongozi wasio halali kuingia bungeni.

Aidha, Mbowe alisema walitaka shughuli ya ufunguzi rasmi wa Bunge isitishwe kwa sasa na kuahirishwa hadi hapo Rais halali aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad, atakapotangazwa rasmi na kuapishwa.

Naye Mwenyekiti Mwenza, James Mbatia, alisema haijawahi kutokea katika historia ya Bunge tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kwa vyombo vya dola kuingia ndani ya bunge na kuwatoa wabunge kwa nguvu.

“Wakati sisi tunatafuta majadiliano mezani ilikumaliza mgogoro huu wenzetu Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameamua kutumia majeshi kukandamiza demokrasia,” alisema Mbatia.

Mbatia alisema kuwa hawatakaa kimya bali wataendelea kupigania matakwa ya wananchi hususan kwa upande wa Zanzibara.

“Kuna mambo mengi yanafanywa hovyo na CCM na wapinzani wamekuwa wakivumilia kwa sababu ya kumpenda mama Tanzania lakini hivi sasa wasijaribu kuharibu amani, utulivu na mshikamano uliopo,” alisema.

Mbatia, alisema kwa kawaida mtu anapodhulumiwa haki yake kila mara matokeo yake anachoka kwa hiyo kuna siku ataifuta haki yake hata kwa kusababisha kumwaga damu.

Naye Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa ) wamesikitishwa na kitendo cha serikali ya CCM kuonesha wazi jinsi walivyobaka na kuikanyaga demokrasia nchini.

Alitoa kauli hiyo aipokuwa akizungumza na mwandishi wetu muda mfupi baada ya kutoka bungeni baada ya kufukuzwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya wabunge wa umoja huo kupinga kitendo cha kuruhusiwa kwa Rais wa Zanzibar kuwa sehemu ya Bunge.

Lissu alisema imeonesha wazi kuwa serikali ya CCM ilivyo kuwa ikitumia mabavu ya kuvunja sheria waziwazi sambamba na kuvunja kanuni za bunge jambo ambalo ni hatari kwa afya ya nchi.

Akizungumzia kutoka kwao nje ya ukumbi wa Bunge alisema serikali ya CCM kwa kutumia kiti cha Spika walionekana kupanga mbinu chafu za kuwazima wabunge wa Ukawa ili wasiweze kufikisha hoja zao mbele za wananchi kupitia bunge hilo.

“Unaweza kuona kwamba serikali ya CCM inavyoweza kuvitumia vibaya vyombo vya dola, kwa utaratibu jinsi ulivyo ili kuruhusu watu waingie katika ukumbi wa bunge ni lazima kutengua kanuni ili watu waeze kuingia lakini kutokana na uovyo na ujinga mkubwa wa serikali ya CCM, ambayo haizingatii sheria na katiba imeweza kuleta askari wengi pamoja na majeshi kwa ajili ya kukabiliana na upinzani.

“Jambo kubwa na baya zaidi na la ajabu ni pale ambapo askali waliovaa magwanda ya polisi na jeshi wakiwa na silaha za moto walivyoweza kuingia katika ukumbi wa bunge kwa misingi ya kutaka kukabiliana na wabunge wa upinzani.

“Jambo hapa ni kwamba hata wao wanajua kuwa Dk. Shein siyo rais halali wa Zanziba lakini kwa ubishi wao wanalazimisha kufanya hivyo na kutokana na hali hiyo ndiyo maana serikali imekuwa ikitumia vyombo vya dola kwa ajili ya kuthibiti wabunge wa Upinzania ambao wametumwa na Umma wasitoe mawazo yao,” amesema Lissu.

Mbali na hilo alisema pamoja na kuwa walizuiliwa kuendelea na bunge, kwa ajili ya kuwasilisha hoja zao kwa watanzania lakini watatumia mbinu nyingi za kufikisha ujumbe kwa jamii kwani kwa sasa kuna kila mikakati ya kuhakikisha wanataka kuuzima upinzani.

Akizungumzia kuhusu kanuni za bunge kwa sasa alisema kama ilivyo katiba ya sasa ilivyo na makosa kibao ndivyo na kanuni za bunge zinavyotakiwa kurekebishwa kwani kuna makosa mengi zaidi.

Kwa upande wao wabunge wa Zanzibar walisema ni dhambi kubwa kwa Dk. Ali Mohamed Shein kuenedelea kung’ang’ania kukaa madarakani wakati muda wake umeisha jambo ambalo linaonesha wazi kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka na dola yake.

“Inasikisha zaidi kuona jinsi Rais wa Zanzibar alivyokuwa siyo muungwana anajua kabisa kwamba hakushinda uchaguzi, lakini ikumbukwe wakati wa kuvunja baraza la wawakirishi wabunge wa CCM walimkataa Maalim Seif Shariff Hamad kama makamu wa kwanza wa rais asiingie katika bunge.

“Lakini kwa uungwana wa kiongozi huyo aliondoka wala hakuhudhuria kikao hicho lakini jambo la kushangaza huyu Dk. Shein amekomaa sasa inafikia hatua anazomewa bila kuwa na aibu sasa huo ni uongozi gani na anamuongoza nani,” amesema.

“Tunamuuliza Rais Magufuli, ni nani akapeleka vifaru na kuongeza askari wengi katika nchi za Zanzibar na ni kwa sababu gani.

“Kwa sasa hali ya Zanzibar si shwali kwani kila jambo sasa limelala kwani hata watalii hawaji kama ilivyokuwa mwanzo, mbali na hilo kuna hali ya sitofahamu ni kwani nguvu nyingi ya vyombo vya dola inaelekezwa Zanzibar,” alisema mmoja wa wabunge wa Zanzibar.
Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo munae mtaja eti ni rais halali alie chaguliwa na wanainchi Zanzibar nani kawambia? kwanza hakuna mtu yeyote anae mfahamu isipokua ukawa peke yake. Na hiyo ni mbinu mlio tumia eti ajitangaz mshind kabla ya umalizaj wa kuhesab kura na tume ya uchaguz ya ZEC kutangaz mshind. Kwan mliona kama Tanzania bara mtashindwa vibay basi mkatumia hiyo mbinu chafu ya kujitangaz wenyew washind, kwanz mungepelekw mahakaman kwa kuvunj sheria ya katib ya uchaguz inao sema kwamb hakun mgombea yeyot atakae jitangaz mshind. Achen vurug tumikien walio wachagua laasivyo mtakion ca mtemakun 2020. Siasa sio kua rais tu wala kutumikia wanainch sio mpaka uwe rais wazir no no no unawez tumikia wanainch bila kua mwana siasa ao kweny cham chochote. tafathali tumikien walio wachagua ili mujiimarish na mue na nguv kwenye uchaguz wa 2020 laa sivyo mtajikut wakat huo huo mnalaumian et nini nani mhusik wala haya yaleee, huo ndo ushaur nawapa wana siasa wa Afrika. Wengin wakishindw huw na nguv ile mbay yakutish ili uchaguz ufuatao wakitoe madarakan cham tawal ila nyiny na wengin Afrika huishia kulalamik, kulet vurugu.

    ReplyDelete
  2. KAMA KWELI UKAWA MNASIMIMIA SHERIA NA MNAZIJUA SHERIA MLIENDA DODOMA KUFANYA NINI? SI MNGEBAKI KWENU MPAKA RAISI WA ZANZIBAR ATANGAZWE, ACHENI UNAFIKI

    ReplyDelete
  3. hahahahahahahahah!!! UKIWA mnatuchekesha kweli, eti mipango yao ya kumzuia Dr. Magufuli asihutubie bunge akiwa na Dr. Shein imefanikiwa!!! hahahahahah ......kwa hiyo ndio kusema nyinyi ukiwa mlibaki ndani ya bunge na Dr. Shein alitoka!!?? na Dr. Magufuli hakuhutubia bunge??!! hahahahahah WATANZANIA-TUNAJUA, NI-UTOTO-NDIO-UNAOWASUMBUA , WAKIKUA-WATAACHA

    ReplyDelete
  4. Hatuwafagilii wala nini, mnakunywa viroba mnaingia bungeni kupiga kelele kama machizi.........mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  5. KWANI BAADA YA YOTE HAYO YA-KIJINGA MLOYAFANYA, NDIO MMEPATA NINI? KAMA NYINYI NI 'WANAUME' KWELI, MBONA MLIPOFUKUZWA MLITOKA NJE? SI MNGEGOMA KUTOKA TUONE .........NYOOOOO......YENU YAMEWASHINDA, MNASHOBOKEA YA ZANZIBAR.....HOVYOOOO

    ReplyDelete
  6. Tanzania ina matatizo makubwa sana, wavuta bangi wamewachagua wavuta bangi wenzao kuwawakilisha bungeni walopigia kura UKAWA wote wanahitaji kuangaliwa akili, Ukawa ni kundi la thugs na yobs si wanasiasa Tanzania nafikiri bado sana kuingia ktk democrasia bado sanaaa nawaoneeni huruma ndugu zangu

    ReplyDelete
  7. Nyinyi UKAWA mnatakiwa ku2mia akili ya kuzaliwa nani kawambia kuwa Dr.Shein cyo rais wa Zanzibar ? Kabla hamjalalamika ilitakiwa msome katiba ya Znzibar ya makwa 2010 na kuielewa? Ttizo ni uhalali wa shein kuwa ni rais halali au uhalali wa mwenyekiti wa ZEC kufuta matokeo? Mbona hamueleweki nyny UKAWA

    ReplyDelete
  8. UKAWA sijui ndio UKIWA hawana hoja wameishiwa wamebakia kuwa wanafiki tu hapa kazi waache usenge

    ReplyDelete
  9. Tanzania kumejaa eajinga.

    ReplyDelete
  10. Inasikitisha sana kama wa2 wenye elimu zao tena wanaitwa WAHESHIMIWA wanafanya mambo hyo utafikiri hawana elimu inakuwaje kwa wananchi ambao hakwenda shule? duuuh inasikitsha sana kuona m2 anaitwa mwanasheria lkn bado anafuata mkumbo ? Duuuuuh UKAWA mna matatizo inatakiwa mjifunze kutokana na kosa mlilolifanya. Mtawaeleza nn wananchi waliowaamini wakawapatia dhamana ya kuwawakilisha au waliwa2ma muwe mnazomea na kufukuzwa bungeni? Jaribu kutambua heshima mlionayo ktk jamii na mambo mnayoyafanya je vinaendana?

    ReplyDelete
  11. Msingepokea posho mnasimulia nini unafiki mtu ,nawaonea huruma waliowachagua ,yaani bora mgenyamaza shame on you Ukawa ,mmetia aibu kasilimulie wake zenu mtupishe ,kusanyeni posho mlizopokea rudisheni ndo tutajua kweli mhamtabui vichwa vya panzi kweli

    ReplyDelete
  12. Watu mil.6 wameichagua Ukawa kati ya mil.8 waliomchaguaJPM kwa mujibu wa tume. Ni bora umesema wazi anony 3.49 PM kuwa Tanzania demecrasia bado ingawa walokutuma wanadai ipo na imekomaa. Ni ujinga kusema waloichangua ukawa ni wavuta bangi wakati rais aliyeko madarakani anatekeleza sera za ukawa. Hakuna mwanasisiem aliyekuwa anawaza kama safari za nje zitafutwa kama sio ukawa kutoa takwimu zilizoonyesha ni jinsi safari za rais zilivyorigharimu taifa mabilioni ya pesa. Nani wa kuvumilia ujinga huo labda nyie wote hapo juu mnaotegemea hisani ya sisiem.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad