Kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili ambao wamehusika na wizi huo.
“Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.
Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru na Bi. Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta Bw. Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.
Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake.
Hii mbona haieleweki vipi wametajwe wafanyakazi tu, itakuaje wafanye peke yao bila wafanyabiashara ambao ndiyo wenye kontena hizo.
ReplyDeleteMbona unaharaka! Mfanyakazi asipowezesha huyo mfanyabiashara atabaki?
ReplyDelete