Ushauri Kwa Rais Dr John Magufuli Kuhusu Kutumia Lugha ya Kiswahili Ndani na Nje ya Nchi Kwenye Mikutano

Ili kuipa hadhi na kuitangaza lugha yetu ya taifa, nashauri rais wetu mpya atumie Kiswahili katika shughuli zote rasmi za kitaifa na kimataifa. Cha msingi ni kuwa na wakalimani mahiri katika shughuli za kimataifa. Hii itainua hadhi na heshima ya nchi yetu badala ya kuendelea kuthamini lugha za kigeni. Tumekuwa watumwa mno wa lugha ya kiingereza mpaka kufikia hatua kudhani kuwa mtu anayeongea kiingereza vizuri ndiye aliye elimika wakati si kweli. Elimu ni uwezo siyo kuongea kiingereza. Hiki kiingereza cha "izi, wozi, wea, kongrugesheni, ameizingi, wati?, yu no, no problemu hakitusaidii kitu. Na kwa ujinga wetu tunafundishana kwa lugha tusiyoijua vizuri matokeo yake watoto wanafeli halafu tunawaona wajinga kumbe sera zetu ndio mbovu. Wachina, wakorea, wajerumani, wareno, wafaransa mbona wanatumia lugha zao na wanapiga hatua kubwa sana katika uchumi na sayansi. Sisi na kiingereza chetu cha kuombea maji tumefika wapi zaidi ya kutudhalilisha?

Maoni yangu haya hayana maana kuwa sitambui uwezo mkubwa wa kiingereza alio nao dr. Nataka aendeleze pale mwenzake alipoachia mwenzake, kwani alianza kwa kuhutubia kwa kiswahili kwenye mkutano wa AU lakini baadaye akaacha. Mimi nashauri Dr. sasa ajikite pamoja na mambo mengi kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa kwa yeye mwenyewe kuitumia badala ya kiingereza. Huwa naona viongozi wa nchi nyingine kama za kiarabu pamoja na kuwa wanajua kiingereza lakini utakuta wanazaunguza kiarabu na kisha wasiojua kutafsiriwa. Wakalimani sasa hivi tunao wengi, ni vizuri wakatumika vizuri kuikuza lugha yetu ya taifa. Ukweli ni kuwa unapotumia lugha mama au lugha ya taifa una kuwa na uhuru na uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuelezea kuliko unapotumia lugha za kigeni. Kwa watanzania wengi lugha yetu ya mama ni kiswahili.
By Tulimumu

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukiwa Tanzania Huwezi kuona umuhimu wa lugha ya kiingereza. Ukitoka nje ya nchi ndio utajua umuhimu wa kiingereza. Kiingereza ni lugha ya dunia, lugha ya biashara, lugha ya utandawazi. Kuongea kiingereza Co utumwa. Kuna nchi Kama China walikuwa wabishi sana kujifunza na kuongea kiingereza. Leo wanaajiri walimu kwa gharama kubwa sana kufundisha kiingereza. Tafuta mambo ya msingi ya kumshauri rais. Kama vile ufisadi na wezi wa kubwa walioko serikalini. Huoni kuwa na mkalimani pia utaongeza gharama kwa serikali Halafu anadhani mtoto wa mkalima atapata nasafi ya kuwa mkalimani. Au ni kuwatengenezea watoto wa Vigogo waliokulia ubalozini ulaji. Think before you write

    ReplyDelete
  2. Hata hii sera ya elimu ya mwaka Jana itawaathiri sana watoto wa maskini. Hakuna kigogo atakae peleka mtoto wake kwenye shule zinazofundisha kiswahili. Kwa vile wanajua madhara yake kimataifa. Baada ya miaka kazaa utaambiwa kupata nafac fulani shart lzma ujue kiingereza. Watoto wao ndio watakao kuwa wenye sifa. Na hivyo kuzalisha tabaka la watawala na watawaliwa. Tuwe makin na jinsi technologia inavyoenda Halafu upime what is important.

    ReplyDelete
  3. Siungi mkono hoja, kwa sababu Tanzania hatuna cja kuringia hadi tutimie Tugha yetu, hatuzalishi chochote watatufuatiria na kumsikiriza kwa lipi?
    China wakiongea kichina wana haki maana tunanunua kutoka kwao, tunawaomba misaada, sasa wewe hata wananchi wako huwexi kuwasaidia ndio uringie kiswahili?

    ReplyDelete
  4. mtoa hii mada kwanza kabisa ni masikini wa akili msishangae, lugha inakuzwa na Rais?? hahahaha maskini tanzania yangu dhaaaa!!

    ReplyDelete
  5. Aongeeeeee kisukuma tutamuelea vizuri

    ReplyDelete
  6. Sawa kabisa ofisi za balozi iwe kazi tutafsiri
    Tuache kuchaguwa watoto WA vigogo kufanya kazi balozini
    Tupo watanzania wengi wenye elimu ughaibuni

    ReplyDelete
  7. ujinga mtupu english haikwepeki ww ujanja ni kuanza toka std one basi

    ReplyDelete
  8. Huwezi kuona wala haitatokea Mchina ,Mrasha,Wananchi wa Amerika Kusini,auMfaransa kuongea Umaja wa mataifa kwa kiingereza wote wana tumia lugha zao,ndio maana kuna watapta(Tranlators)
    Kiswahili ni muhimu.
    Msimbazy

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nazan ww hufuatilii mikutano ya kimataifa. Hata msiba wa Mandela utakusaidia kujua ni nchi ngapi zilitoa speech kwa lugha yao. Ni China tu na bado walitumia mda mwingi maana walikuwa wanaongea wawili. Kidiplomacia utaizika nchi yako. Usijilinganishe na nchi Kama China au urusi au ugerumani. We sera ya nchi yako inahitaji wawekezaji wao hawahitaji wawekezaji wala wataalam. Tembea ujionee ndugu yangu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad