Wabunge Wateule Waitwa kwa Dk Magufuli....Watakiwa Kufika na Cheti Kinachoonyesha Kuteuliwa Kuwa Mbunge

John Magufuli
Wabunge wote wateule, wametakiwa kufika Ofisi Ndogo ya Bunge Dar es Salaam, ili kushiriki hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule, Dk John Magufuli.

Wabunge hao kutoka majimbo 259 nchini walichaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili ya Oktoba 25, ambao pia ulimpa ushindi Dk John Magufuli wa CCM, dhidi ya mshindani wake wa karibu Edward Lowassa wa Chadema aliyeungwa mkono na Ukawa.

Akizungumza jijini hapa  leo, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema wabunge hao wateule wanatakiwa kuwasili kwenye ofisi hizo,  kila akiwa na cheti  kinachoonyesha   kateuliwa kuwa mbunge, kilichotolewa na  msimamizi wa uchaguzi wa jimbo husika.

Cheti hicho, kitawasilishwa kwa maofisa wa Bunge wakati wa zoezi la usajili, pia kila mbunge mteule atatakiwa kubeba kitambulisho kingine chochote kilichotolewa na mamlaka inayotambulika, kinachoonyesha jina lake kamili kama lilivyoandikwa kwenye cheti cha ubunge,”alisema Joel.

Ameongeza: “Uchaguzi umekwisha, lakini baadhi ya majimbo bado kutokana na sababu mbalimbali. Masikio ya wananchi na wabunge wateule ni kujua nini kitafuata upande wa ofisi ya Bunge, ndiyo maana  leo (jana ), tunatangaza kuwaita   wateule wote kufika  Dar es Salaam Novemba 4 mwaka huu.

Amefafanua kwamba usajili kwa wabunge wote wateule utafanyika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma na kila mbunge atajitegemea usafiri kwa ajili ya shughuli hiyo itakayofanyika kabla ya kuanza kwa Mkutano  wa Kwanza wa Bunge la 11.

Kuhusu kuongezeka kwa majimbo, Joel alisema wamejipanga na kuongeza viti ili kuhakikisha wabunge wote wanapata nafasi ya kuketi kwenye ukumbi huo.

Hatujabadilisha ukumbi  bali tumeongeza idadi ya viti kwa kazi mbili maalumu .Moja ni kwa ajili Rais atakapozindua Bunge na pili   kwa wabunge wote wakiwamo wa viti maalumu, ambao bado hatujua idadi yao,” alisema Joel.

Kwa mujibu wa Joel, mkutano huo wa kwanza unatarajiwa kuanza siku ambayo Rais ataitisha Bunge na utahusisha  uchaguzi na kiapo kwa Spika, viapo kwa wabunge wote wateule, kuthibitisha jina la Waziri Mkuu, uchaguzi wa Naibu Spika na  ufunguzi rasmi wa Bunge la 11.

Joel alitumia nafasi hiyo kuvikumbusha vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu vilivyo na nia ya kusimamisha mgombea uspika kuanza mchakato  mapema kwenye ngazi ya vyama,   kabla ya tangazo la nafasi ya Spika kuwa wazi.

 Amesema lengo la kuvikumbusha ni kuvitaka vikamilishe mchakato kwa wakati na kuwasilisha jina la mgombea kwa Katibu wa Bunge.

 DONDOO

Spika anaweza kutokana na wabunge au mwanachama wa chama cha siasa ambaye jina lake liliwasilishwa kwanza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kujiridhisha kama ana sifa za kuwa mbunge



Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  2. HUU NI MWANZO MBAYA,MWANZO MCHAFU,MWANZO WA KIHUNI WA KEJELI KUTOKA KWA HAWA WEZI WAKUBWA WA KURA CCM.LAKINI,MUELEWE BUNGE LA SAFARI HII SI LILE MLILOLIZOEA.HAPA KUNA MOTO WA KUOTEA MBALI.KWANZA IDADI YA WABUNGE WA UPINZANI ITAONGEZEKA SANA TOKA HAWA 84 WALIOPITA HADI 106,ONGEZEKO LA WABUNGE WA UPINZANI WAPATAO 22.PILI RUFAA ZINAZOPELEKWA MAHAKAMANI ZAIDI YA 40 NYINGI TUNATEGEMEA ZITAJIBU KWA SABABU NI HALALI KABISA.TATU SAMPULI YA WAPINZANI WANAOINGIA BUNGENI,BALAA,UTAMWAMBIA NINI BULAYA,LWAKATARE,TUNDU LISSU,MTULIA,HALIMA MDEE,SUGU,PROFESA J,MWITA MARWA, MATIKU ACHILIA MBALI HEAVYWEIGHTS MBATIA,MBOWE NA WENGINEO WAKALI WENGI,WENGI.106 NI KIJIJI ,NYINYI JIZODOENI TUU. HUU NI WEMBE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad