Walisema Hataweza Kuleta Mabadiliko Ndani ya Mfumo wa CCM, Sasa Wanadai Anatekeleza ilani yao

Hawa marafiki zetu wa upinzani kwa maoni yangu ni watu wa kutafuta tafuta sababu za kujitetea!
Wakati CCM inampitisha Magufuli kuwa mgombea urais, jamaa wakajaribu kuja na hoja kwamba hata aje malaika hataweza kuleta mabadiliko Kwasababu ya mfumo uliopo!!

Hoja yao ikawa Magufuli anafaa kuwa Raisi lakini mfumo ulio chini ya chama cha Mapinduzi utakuwa kikwazo kwake kuleta mabadiliko ambayo Magufuli alikuwa akiya nadi wakati wa kampeni! Ajabu ni kwamba hawakutuambia wakati ule kwamba mabadiliko aliyokuwa anayanadi Magufuli wakati wa kampeni yako kwenye ilani yao. Wao walichokiona na kutuaminisha wananchi ni kwamba ilani ya CCM iliweka mabadiliko ambayo Magufuli atashindwa kuyaleta akiwa ndani ya mfumo huu!!
Kichekesho sasa!!!

Baada ya wananchi kutokuwaamini wapinzani na kumuamini Magufuli na wakamchagua kuwa Raisi.
Na Magufuli huyo akaanza kuzifanyia kazi zile ahadi za mabadiliko alizozitoa wakati wa kampeni, wale jamaa wanarudi tena na hoja nyingine,
Eti Magufuli ameamua kuifuata ilani yao na kuiacha ilani ya CCM aliyoinadi!!!
Hivi hizi ni akili timamu kweli????
Wamesahau kwamba wakati Magufuli akiinadi hiyo ilani wakati wa kampeni, hao hao waliiona ni nzuri lakini wakajaribu kuwaaminisha watz kwamba Magufuli atashindwa kuitekeleza Kwasababu ya mfumo!!

Leo Magufuli anawaonyesha kwamba mfumo hauwezi kumzuia kuitekeleza ilani hiyo ya CCM na mabadiliko iliyoya ainisha, wanasema hayo unayo yafanya yako kwenye ilani yetu!!!!
Hivi mabadiliko Yale mliyo sema atashindwa kuyaleta Kwasababu ya mfumo ni yapi????
Magufuli amewathibitishia kwa vitendo kwamba siku zote mko wrong!!!!
Inabidi mfikirie tena!!!!

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwahiyo sisi tufanyeje,.. mabadiliko ni kwa faida ya watanzania wote yawe yameletwa na ukawa au ccm tanzania ni moja rais ni mmoja hakuna haja kuandika mada za kinafiki.

    ReplyDelete
  2. Nimeipenda mada yako lakini sijakuelewa, kumbuka katika mashindano yoyote mambo hayo hutokea na ni lazima upambane kwa hoja nyingi. Lakini kwa nini kuendelea na siasa wakati huu ni wa kujenga taifa ambalo hata wewe unaona misingi ya haki za binadamu ilishakiukwa na kushikwa na watu wasiowatakia mema wanyonge? Mtazamo wangu wapinzani walikuwa na haki katika mashindano yale na bado wanahaki kusema wanachotaka kusema. Lakini sisi watazamaji tufanye kazi. Asiye fanya kazi asile! pia sheria yetu inasema Raisi akishatangazwa na tume ya uchaguzi huyo ndio Raisi. sasa Tumuunge mkono malumbano hayana nafasi sasa.

    ReplyDelete
  3. Alieandika Makala atakua katumwa Na Zitto Kabwe

    ReplyDelete
  4. Tu kumbukumbu pia watu walikuwa wanapima wagombea na siyo chama. Kama chama ccm kulikuwa hakina sifa na ndiyo maana hata wakati wa kampeni watu walikuwa wanamnadi magufuli na Co ccm.

    ReplyDelete
  5. mpaka sasa hv ccm haina sifa, huyu watu wanamchukulia ni mtu mchapakazi ndiyo maana anakubadilika mpaka na wapenzani, binafsi ingekuwa taamu kweli kama wabunge wengi wangekuwa wa upenzani na huyu ndiye raisi, hapo nadhani watanzania wangefaidika Zaidi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na hilo ndosa wa lilo Fanya wapinzani kusahau kuwasaidia kampeni za wabunge na kuwa busy na edo. Matokeo yake tumewapoteza wabunge mahiri Kama kafulila, machali na wale wa mwanza. Kwa kweli upinzani walitakiwa wajikite zaidi kwenye nafac ya ubunge kuliko kutoa raisi. Kulikuwa kunachangamoto kubwa kumpima raisi wetu na edo ktk usafi wao. Lkn yameshapita sasa tumsaidie raisi kutumbua majipu. Anaonesha anania ya dhati.

      Delete
  6. MALOFA NA WAPUMBAVU LAZIMA WAWAZE HAYO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad