Watanzania Wenzangu Tumombee Rais Wetu Kutokana na Hizi Changamoto Kubwa Kwake

Ninawaomba watanzania tumwombee Rais wet mheshimiwa Magufuli kutokana na changamoto zilizo mbele yake. Ninajua Magufuli ana moyo wa dhati kuwatumikia watanzania lakini yafuatayo ni changamoto kubwa kwake.

'1. Chama chake. Chama chake ni mzigo na yeye si mwenyekiti. Lolote akaloamua chama kinaweza kukataa na hawezi kufanya chochote. Kwa jinsi hii mabadiliko ya Magufuli ni ndoto, Hayo yatamshosha Magufuli upesi sana.

2. UKAWA. Kwa hali halisi Ukawa wana wanachama wengi sana na mpaka kesho wanaamini Lowassa ndiye rais Hii ni changamoto kufanya na watu wasiokukubali. Itabidi utumie nguvu kubwa sana kuwatawala.

3. Uchaguzi wa Zanzibar. Ninafikiri mambo ya Zanzibar yanamuumiza kichwa kama yanavyotuumiza na sisi

4. Kutekeleza ahadi zako ambazo kwa uhalisia wa chama chako hazitekelezi.

Kutokana na haya mambo ninaona utawala wa Magufuli ukiwa mgumu kwa wakati huu wa mwanzo ndiyo maana watu wanaotakia nchi yetu mema inabidi tumombee hili Mungu ampe hekima katika kukabiliana nayo.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Magufuli alisema yeye hataki kua mwanasiasa siasa atawaachia watu wengine yeye ni kazitu

    ReplyDelete
  2. Makala pumba kabisa na ni umbavu wa kudhani kuwa kuna watu wanaoamini Lowasa ni raisi. Kwa kujifurahisha wanaweza kuamini hivyo lakini mambo hayo hutokea kwa waafrica peke yao. Na ukichunguza hao watu wanaoamini kuwa lowasa raisi ni watu wa tabaka lake la karubu sasa huo ni ujinga watanzania wanapaswa kufahamu kuwa vyama vya siasa barani Africa hasa vya upizani kutokana na uweledi wao mdogo katika mambo ya siasa vimepelekea kulazimisha mambo ambayo kimsingi hayawezekani kwani hawana nguvu nayo kisheria na mara nyingi hutumia vurugu kama njia moja wapo ya kudai madai haramu. Leo wanasema raisi sio mwenyekiti wa chama kwa hivyo atakuwa hana nguvu? Wakati miaka nenda miaka rudi wapinzani hao hao walikuwa wakilalamika kuwa haiwezekani kuwa raisi wa nchi awe huyo huyo mwenyekiti wa chama? Sasa jiulize nini hasa wapinzani wanachokitaka kama si vurugu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nafikiri dugu yangu unao upeo mdogo sana katika mambo ya siasa za afrika ni bora unyamaze kimya lakini kwa ufipi ni kwamba vyama vilio madalaka vina uchu wa madaraka na havitaki kukuza demokrasia na usawa kwa ajori ya manufaa ya nchi yetu na afrika kwa ujumla angalia kenya mpaka watu waliuwana ndiyo chama pinzani kuingia madarakani mseni uganda mpaka leo kang'ang'ania mpaka watu wauane Burundi na sehemu nyingine nyingi, mabadiliko ya kweli na maendeleo ya kweli ni ndoto kwa bara la afrika kama vyama tawala tena vizee vikongwe havita kubali kuruhusu demokrasia ikue na watu wenye fikra pevu kuingia kwenye utawala

      Delete
  3. Tukumbuke kuwa ukicheka na Nyani utayavuna mabua. UKAWA wanataka kuleta machafuko na si mabadiliko yenye lengo la kujenga kama wanavyoaminisha watanzania, hili lipo dhahiri wanahitaji kudhibitiwa mapema. HAKUNA WALICHOTANGAZIA WANANCHI WAKAONEKANA KUJIPANGA KIKAMILIFU ukianzia namna walivyompata mgombea wao, mikutano yao ni kama watu fulani ambao wanakutana kidharula tu, Hawapendi kukosolewa wala kuangalia wapi wamekosea ili warekebishe wao ni lawama lawama na KUONEWA tu kila siku TUMEWACHOKA MSITUVURUGE AKILI uchaguzi umeisha tuacheni wananchi tufanye kazi za maendeleo ya watoto wetu nyie watoto wenu tayari wameshatoka kimaisha, KAMA HAMUWEZI KUWATUMIKIA WANANCHI WALIOWACHAGUA basi kachungeni Ng'ombe waachieni wenzenu wafanye kazi, tangazeni wazi kwa wananchi kwamba hata mshahara atakaowapa huyo msiemtaka hamtapokea ili BASI TUONE HUU UZALENDO WENU.

    ReplyDelete
  4. Katika nchi za wenzetu mgombea akishinda robo tatu ya kura za mshindi ana haki ya kushiriki katika uongozi kwani watu mf.6mil walompa kura Lowasa wanatosha kuleta vurugu na kuifanya nchi isitawalike. Nadhani hiyo ndo concept ya mwandishi

    ReplyDelete
  5. HUYO ALOKUTUMA KAMWAMBIA TUMSIKIA LAKINI HATUKUMWELEWA, MKAJIPANGE UPYA.........HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad