Watu Sita Wapoteza Maisha Katika Ajali ya Gari Morogoro

Watu sita wamefariki dunia baada ya gari ndogo waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria mali ya kampuni ya Princess Muro, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma, katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro-Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, ikihusisha gari ndogo la abiria aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 359 BBA iliyokuwa imebeba abiria sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne ambayo ilipasuka tairi ya Mbele ya kuyumba ovyo barabarani na kugongana na basi hilo la Princess Muro lenye namba T 160 BBC na kusababisha vifo kwa abiria wote wa Noah.

Amesema basi hilo la abiria aina ya Zangton lililoharibika zaidi mbele huku Noah ikiharibika kabisa, likuwa likiendeshwa na Silos Wilfred (55) mkazi wa Mbeya ambaye anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na kwamba basi alilokuwa akiendesha lilikuwa na abiria 59 ambao hawakupata madhara makubwa, isipokuwa michubuko kidogo kwa baadhi yao na walitafutiwa usafiri kuendelea na safari.

Katika upekuzi wa miili ya abiria waliokuwa kwenye Noah inayodaiwa kuhusika na ubebaji wa magazeti, viligundulika vitambulisho vimne vya Ali Nduti Mohamed (27), mkazi wa Mbeya,Sani Elion Mkwabe (24) mkazi wa Kunduchi, Patrick Mkelegene (43) mkazi wa Buguruni Malapa na Selemani Omary (30) ambaye makazi yake hàyajaweza kujulikana Mara moja.

Miili ya watu hao waliopoteza maisha imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo kubwa za hizo ajari ni barabara za kiwango cha chini sana kunabidi kuwe na divider kwa magari ya pande tofauti kwani ni barabara za mwendo kasi highway hilo lilibidi lizingatiwe

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad