Hofu imetanda kwa watuhumiwa wa kesi za matumizi ya madawa ya kulevya waliopo katika magereza mbalimbali nchini, kufuatia hukumu kali iliyotolewa hivi karibuni katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Mnaijeria Chukwudi Okechukwu na wenzake watatu Paul Ikechukwa Obi, Shoaib Muhammad Ayaz na Hycenth Stani.
Wanne hao walihukumiwa na Jaji Amir Rajabu Mruma wa Mahakama Kuu kwenda jela kwa miaka 30 na kulipa faini ya bilioni tisa ikiwa ni mara tatu ya thamani ya kilo 81 ya dawa za kulevya aina ya Cocaine walizokamatwa nazo zilizokuwa na thamani ya shilingi bilioni tatu za Kitanzania.
Jaji Mruma alitoa hukumu hiyo kwa kuzingatia Sheria ya dawa za kulevya namba tisa ya mwaka 1995 ambayo inasema kuwa mtu akikamatwa kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya atafungwa kifungo kisichopungua miaka 20 na kutakiwa kulipa faini mara tatu ya thamani ya dawa alizokamatwa nazo.
Inadaiwa kuwa watuhumiwa wengi wa kesi za dawa za kulevya, hutumia fedha nyingi kukwepa hukumu kwa kuwahonga majaji na mahakimu wanaokuwa wakizisikiliza, hivyo kitendo cha Okechukwu na wenzake kuhukumiwa kwa miaka mingi kimeibua hofu kubwa kuwa inawezekana kuanzia sasa hukumu zikawa ni kali sana.
Hofu inazidi wakiangalia mwenendo wa hukumu za madawa ya kulevya za hivi karibuni ambapo baadhi ya waliohukumiwa ni Bakari Kileo Bakari alihukumiwa miaka 25 jela na faini ya shilingi bilioni saba na mia mbili, Kadiria Said Kimaro, miaka 20 na faini ya milioni 144 wakati mtuhumiwa Fred William Chonde akihukumiwa miaka 20 na faini ya shilingi bilioni 15 na milioni 600. Wote hawa walikutwa na hatia za kukamatwa na madawa ya kulevya.
Wakizungumzia hukumu hiyo baadhi ya wananchi waliipongeza ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP) wa Serikali kwa kuhakikisha kesi za madawa ya kulevya zinashughulikiwa kwa kasi na kuitaka iboreshe zaidi utendaji wake.
Tatizo hili la madawa ya kulevya limetuathiri kwa muda mrefu, kwa hiyo zinapotolewa hukumu kali kama hizi zinasaidia kuwapunguza kasi wafanyabiashara wa dawa hizo,? alisema Juma Khamis, mkazi wa Kariakoo Dar es Salaam.
Naye, Mwanaidi Hassan mwanafunzi katika Chuo Cha Mwalimu Nyerere, alitaka jitihada za udhibiti ziongezwe ili kuwaepusha vijana wasiathiriwe zaidi na madawa ya kulevya.
Tunahitaji hatua kali zaidi. mahakimu watoe hukumu kwa kuzingatia Sheria na kusiwepo mianya ya rushwa kwasababu tatizo hili litatumalizia nguvu kazi.?
Watuhumiwa wa Madawa ya Kulevya Bongo Waingiwa Kiwewe
2
November 23, 2015
Tags
HAPA KAZI TU...........KAZI...........KAZI..........KAZI TU!!!
ReplyDeleteindonesia wanapiga risasi hiyo mbona adhabu ndogo,msiwahurumie hawa wanatuulia ndogu zetu au nyie hamuoni ilo
ReplyDelete