Wazanzibari Wanaoishi Uingereza Waandamana Wakitaka Maalim Seif Sharif Hamad Atangwe mshindi wa Kiti cha Urais

Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza jana walifanya maandamano wakidai haki ya kutangazwa ushindi wa Chama Cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Octoba 25 mwaka huu

Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association (ZAWA) ambapo wazanzibari hao walitoka maeneo mbali mbali katika miji yao na kukusanyika katika eneon la  Downing Street kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na uongozi huo kukabidhi barua yao yenye malalamiko kutaka suala la Zanzibar lishughulikiwe.

Maandamano hayo yalifanyika kwa lengo la kuongeza shindikizo kwa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua za haraka ya kuhakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inakamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Zanzibar  iliingia katika mkwamo wa kisiasa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha Octoba 28 kutangaza kuufuta uchaguzi wote kwa madai kwamba ulikumbwa na matatizo mbali mbali.

Wakati jecha akitoa tangazo la kufuta matokeo bila ya kushauriana na tume yake alikuwa tayari ameshatangaza matokeo ya kura za urais za majimbo 31 kati ya 54 ya Zanzibar pia washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani katika majimbo hayo walishatangazwa na walishakabidhiwa vyeti vyao.

Rashid Ali ambaye ni kiongozi wa ZAWA  alisema jana kuwa wamewasilishwa barua hiyo wakiamini kwamba suala la Zanzibar litashughulikiwa ili wananchi wa Zanzibar waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Mwakilishi wa ZAWA, Hassan Khamis alisema wameamua kupeleka barua kwenye ofisi za waziri Mkuu wakiamini suala hilo litashughulikiwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti na za haraka kaika kushughulikia suala hilo ambalo limewaweka wazanzibari roho juu.



Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao si wazanzibar bali tayari wana uraia wa uingereza,wengi nimewaona katika hiyo picha nawaafahamu vizuri wameshaukana utanzania!Watuachie nchi yetu wao waendelee kula bata huko kwa malkia!

    ReplyDelete
    Replies
    1. aliyekuambia wewe hii ni chi yako ninani? na uanze waambia wengine hii siyo nchi yao? umechanganyikiwa wewe!

      Delete
  2. Musiwe na wasi nyie wazanzibari ccm ndio itaongoza nchi kwa ajili ya amani na itulivu wa nchi yetu. Nyie munataka cuf ipepewe madaraka ili mulete dhambi za ubaguzi mutaanza kupigana vita wapemba na wa unguja

    ReplyDelete
    Replies
    1. CUF waliharibu walipo ropoka hovyo kuwa wanataka kuvunja muungano. Mi naona tuwatenge tu maana sijaona faida yao, wakalelewe na inchi za kiarabu.

      Delete
    2. CUF waliharibu walipo ropoka hovyo kuwa wanataka kuvunja muungano. Mi naona tuwatenge tu maana sijaona faida yao, wakalelewe na inchi za kiarabu.

      Delete
  3. BASI NYIE CCM MUSIFANYE UCHAGUZI KAMA HAMKO TAYAR KUWACHIA NCHI MUNATIA HASARA TAIFA THEN ALIESHINDA HAPEWI HAKI YAKE

    ReplyDelete
  4. TUKIAANZA KUBAGUANA KWA ASILI CCM MTAWEZA?WEWE UNAYESEMA HAWA SIO RAIA TUTHIBIISHIE URAIA WAKO PIMBI MBWA WEWE.ULILETWA LINI UKAFIKIA WAPI MNYASA WA CHIWILE MZUZU.KOMA TENA UKOME KUROPOKA ACHA WAZANZIBAR WAIAMBIE DUNIA,NA,WATASEMA

    ReplyDelete
    Replies
    1. umekosa hoja unaishia kutukana, ndio maana mlinyimwa chogo so hata akili zenu fupi pia.

      Delete
  5. MUTARUDISHWA UTUMWANI NA CUF

    ReplyDelete
  6. mwarabu gani mwenye shida na Zanzibar mbovu naona nyie mnatoka hapa mnaenda kutumwa OMAN kazi za majumbani, supermarket, kukata majani n.k. mmeanzisha campuni ya kusafirisha wenzenu kwenda huko, kinachozungumzwa ISICHUKULIWE HAKI IKAFANYWA BATILI NA MUNGU HAYUKO RADHI NA HILO.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad