Zitto Kabwe Ayafungukia Makampuni Makubwa Tanzania Ambayo Yanakwepa Kodi....

By Zitto Kabwe
Kutoka Hotuba ya Waziri Mkuu 26.08.2011 – Makampuni yanayoogoza kwa kulipa kodi

Note: (Highlights)
Only one Mining company (the smallest i.e. - Resolute Mining), only one telecom company(Airtel Tanzania).
Household names like: 
MeTL, Bakhresa/Azam, IPP, VodaCom, Coca cola, Pepsi(SABCO), Serengeti Breweries, Barrick Gold, ACACIA, AngloGold Ashanti not seen. No oil marketing companies pia.
One can conclude that, TBL is the most profitable company in Tanzania, NMB is the most profitable Bank.
A public debate is needed. Hili ni tatizo kubwa.
Here under is the an extract from the Prime Minister speech; Sehemu ndogo ya hotuba ya Waziri mkuu.
Mheshimiwa Spika,
1. Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:
  1. Tanzania Breweries Ltd. (Tshs 165.4b)
  2. National Microfinance Bank (Tshs 108.6b);
  3. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);
  4. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);
  5. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);
  6. Tanzania Ports Authority (Tsh 76.8b);
  7. Tanzania Portland Cement (Tshs 73.4b);
  8. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);
  9. Tanga Cement Company Ltd. (Tshs 43.6 b);
  10. Standard Chartered Bank Ltd. (Tshs 40.0b );
  11. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);
  12. Resolute (T) Ltd. (Tshs 32.1b );
  13. Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);
  14. Tanzania Distillers Ltd. (Tshs 13.4 b); na
  15. Group Five International (PTY) Ltd. (Tshs Bilioni 9.5).

2. Napenda kutoa rai kwa Makampuni yote Nchini kuiga mfano huu mzuri. Wito wangu kwa Makampuni, Wafanyabiashara Wakubwa kwa Wadogo na Wananchi wote ni kuongeza juhudi katika kufanya biashara zao ili zizalishe kwa wingi na kupata faida kubwa zaidi. Faida kubwa itachangia katika kuongeza Mapato ya Serikali kwa njia ya Kodi na hivyo kusaidia kukuza uchumi, kuongeza Pato la Taifa na la Mwananchi mmoja mmoja na kuondoa Umaskini. Niwadhihirishieni kwamba, Serikali inatambua umuhimu wao kwa maendeleo ya Nchi yetu na itahakikisha inaongeza juhudi zake za kuweka Mazingira Wezeshi kwa Makampuni hayo kufanya shughuli zao vizuri ili kuwezesha kulipa Kodi kwa mujibu wa Sheria.
Issues, issues, issues

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HII NI TAARIFA YA MWAKA 2011,ZIMEPITA SIKU.HUWEZI MHE.ZITTO UKAITUMIA TAARIFA HII KUONYESHA PICHA YA SASA 2015.MIMI NINAVYOFAHAMU KUTOKA TRA BASE YEAR 2014 IPO ORODHA A YA MAKAMPUNI YA WALIPAJI KODI WAKUBWA MIA TANO [500].ZITTO AMETANGULIZA 15,NO NI MUONGO,NI MNAFIKI,NI MCHONGANISHI.SERIKALI YETU INAPASWA KUWA MAKINI SANA NA MAHUSIANO MEMA YA KIUTENDAJI NA MAKAMPUNI NA WAFANYABIASHARA WOTE NCHINI TANZANIA.INAVYOONEKANA SERIKALI YA SASA HAIUTAMBUI MCHANGO WA SEKTA YA BIASHARA NCHINI NA MTAFARUKU WOWOTE BAINA YA DOLA NA WATUMISHI WA SERIKALI WA KUKUSANYA MAPATO YAKE YAANI TRA UZINGATIE ZAIDI WIZI WA BAADHI YA WATUMISHI WA TRA NA MWAJIRI NA SI MAKAMPUNI YA BIASHARA.UMENIKADIRIA KODI NIMELIPA,SASA UNANIAMBIA NINI? .WACHUNGUZWE,WACHUKULIWE HATUA,HIYO NI SAWA TUU.LAKINI KUANZA KWA MAKUSUDI KUYAVUNJA MOYO,KUYAPA VITISHO,KUYAHUJUMU MAKAMPUNI YETU MAKUBWA YA BIASHARA,HILO TUNALIKATAA NA KULILAANI KWA NGUVU ZOTE.IKUMBUKWE MCHANGO WA MAKAMPUNI HAYA KWENYE PATO LA TAIFA NI ZAIDI YA ROBO TATU YA UJUMLA.UCHUMI WETU UTAYUMBA NA UUNGWAJI MKONO SERIKALI UTASHUKA SANA.RAIA TUNATAKA MAENDELEO NA SI VINGINEVYO.MAKAMPUNI HAYA YAMEWAAJIRI MAMILLIONI YA WATANZANIA NA WOTE KWA NJIA MOJA AU NYINGINE TUNAFAIDIKA.MTAJE BAKHRESSA KWA MFANO MDOGO,NI NANI HAFAIDIKI NAYE?LEO UNAMWANDAMA KWA KUMUONEA,NANI ATAKUUNGA MKONO.TUNALAANI MANYANYASO YEYOTE KWA WAFANYABIASHARA,AWE MKUBWA AWE MDOGO.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli,naunga mkono.TRA ni wataalamu waliobobea wa wa kodi.wamesoma na wana uelewa woote wa mifumo ya kodi[ A to Z].makadirio ya kodi yanayofanywa TRA kwa wafanyabiashara ni kwa kulingana na mifumo yao.mwisho wa siku napewa hesabu naenda benki nalipia napata tax clearance.leo hii niandamwe mimi mlipa kodi.nilijikadiria? nauliza nilijikadiria? KIMSINGI, TRA NI WEZI WAKUBWA KULIKO HATA EPA NA ESCROW UKIZIWEKA PAMOJA.lakini hili ni baina yao TRA na mwajiri wake yaani SERIKALI.msiwanyanyase wafanya biashara,ni makosa makubwa.

    ReplyDelete
  3. Hivi Zito kakosea wapi jamani? Yeye pia ka declare kwamba data anazozitoa ni za 26.08.2011 sasa utamlazimishaje kutumia 2014 kama base year wakati hafanyi Financial Statement Analysis? Jamani tuwe fair tunapojadili mada

    ReplyDelete
  4. Anonymous 9.33 wala hata usijifanye hujui ni namna gani mfanya biashara aliweza kukwepa kodi sahihi,(UNAJUA kwa 100%)Ila wewe ni mmoja kati ya wale wasiokubali serikali ya awamu ya 5 kwamba iko makini.Umekadiriwa sawa,na pengine kwa makusudi umemtaka afisa wa TRA atumie mfumo wao,(wenu),kwani hukutoa chochote(mgao) kwa afisa wa TRA?

    ReplyDelete
  5. Sasa nani asiyejua kuwa wafanyabiashara baadhi, wanapewa evaluation ya kulipa kodi ndogo kwa kuhonga kwanza? Hicho ndio kinachofanyiwa kazi, mtu badala ya kulipa tax ya mfano shs 100m kwa mwaka, anakadiriwa kulipa 30m kwa mwaka halafu mtu anatupia mfukoni kama 20m, hana hasara, wewe Anonymous wa kwanza kuchangia unataka ushenzi huu uendelee mpaka lini? nchi hii siyo ya wajanja wachache wezi wezi wa kujinufaisha wao na familia zao kwa kuwanyonya wengine, Magufuli na awamu ya tano tunawaombea Mungu waendelee, awamu ya 4 ndio imetufikisha hapa na baadhi ya watu wanataka ushikaji tu, ukishindwa biashara kwa kuwa mpaka ukwepe kodi acha, mbona wafanyakazi hata anayelipwa 1m kwa mwezi analipa kodi bila kupunja, wewe mfanyabiashara ni nani ukwepe? Haki kwanza na maslahi ya taifa kwanza, tuache mambo ya ubishi wa kijinga tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad