Zitto Kabwe Yamemfika Hapaa! Ataka Zanzibar Itangaze Matokeo ya Uchaguzi na Mshindi Aapishwe...

Mbunge mteule wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar yatangazwe na mshindi aapishwe.Zitto Kabwe amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kudai kuwa suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa kwani hawawezi kutazama Katiba ikikanyagwa, vinginevyo amesema Maalim Seif apate Jaji amwapishe na aunde Serikali mara moja.

"Suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa. Matokeo yatangazwe na mshindi aapishwe. Hatuwezi kutazama tu Katiba inakanyagwa. Vinginevyo Maalim Seif apate Jaji amwapishe na aunde Serikali mara moja na kuanza kuwatumikia Wazanzibari, Serikali ya Umoja wa kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar" Amesema Zitto Kabwe

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha. Mnamo tarehe 28 Oktoba alitangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi Zanzibar, uliofanyika Oktoba 25, 2015.


Jecha alisema kuwa, ZEC imefuta matokeo ya uchaguzi kutokana na kukiukwa kwa sheria na taratibu mbalimbali za uchaguzi wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo. Na kutangaza Uchaguzi huo kurudiwa.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UMEZUNGUMZA SUALA LA MAANA WABUNGE KAMA NYIE MNAOTETEA HAKI NA SHERIA NI WATU MUHIMU KATIKA TAIFA LETU. SUALA LA ZANZIBAR NI MUHIMU KUSHUGHULIKIWA SIO KURUDIA UCHAGUZI HALINA NAFASI WALE TEAMS SHENI HAWANA USOMI WALA AKILI WAMEKALIA UBAGUZI TU TENA WA UPEMBA RAIS NI RAIS TUWACHE HAYO HALI YA MAISHA IMEZIDI KUWA NGUMU ZANZIBAR JAMANI MAGUFULI IIYONE HALI HII.

    ReplyDelete
  2. Mh. Zitto kwanza nilisikitika sana wewe kutengana na CHADEMA na mpaka sasa huwa nafsi inaniuma. Wewe, Mh. Joshua Nasari, na aliyekuwa Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe, Kafulila, F. Mkosamali na wengine wachache MLIKUWA VIJANA CHACHU YA MABADILIKO YA MFUMO MBOVU ULIODUMU KWA ZAIDI YA MIAKA 50 na, ninaamini kama si ukiritimba uliokuwepo (japo naamini Mh. Rais atasimamia HAKI YA WATANZANIA) na hatimaye kuuondoa, nyie ndio WATU MNAOTAKIWA KATIKA TAIFA HILI KULETA MABADILIKO YA KWELI. Inaniuma saaana DEO hatunae, Mwenyezi Mungu amlaze pema peponi. Nyie mliopo unganisheni nguvu zenu tena ili kuijenga Tanzania ya WATANZANIA WOTE na si ya WACHACHE. Safi sana kuliona hilo la Seif Hamad. Hongera sana kaka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi wewe unayezungumzia mfumo mbovu uliodumu zaidi ya miaka 50, unamiaka mingapi? Au unafuata mkumbo tu? Hatakama ni kutaka mabadiliko ndio yataletwa na Lowasa?? Katika hiyo miak 50 huyo Lowase wenu hakuwepo?? TAFAKARI, CHUKUA HATUA

      Delete
  3. Sio lazima kuapishwa na jaji, hata mke wake anaweza kumuapisha na akaanza kazi Ikulu mara moja, kama alivyofanya Mwai Kibaki

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad