Aliyekuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dr Edward Hosea, anatarajiwa kutapika cheche wakati wowote kuanzia sasa kwa lengo la kutumbua majipu ya vigogo wa serikali na makada waliokuwa wakimfunga mikono na miguu wakimzuia kufanya kazi yake kwa ufasaha na umakini unaotakiwa.
Katika cheche zake hizo, mtaalamu huyo wa masuala ya rushwa na ufisadi, ataweka hadharani majina ya vigogo na makada wa chama waliokuwa wakimchimba mkwara na kuwaachia wafanye yao ili kulinda kibarua chake tukufu.
Katika orodha hiyo ya Dr Hosea wamo watu wazito kutoka serikalini waliokuwa wakimuandikia vimemo mara kwa mara wakati wanapopitisha makontena yao bila kulipia ushuru na kuikosesha serikali mabilioni ya shilingi za mapato.
Aidha, inasakikiwa kwamba kwenye orodha pia wamo wauza unga na majangili wakubwa waliokuwa wakipitisha unga na vipusa mtawalia, kupitia banadari ya Dar es Salaam bila kuguswa na mtu yeyote. Pia wamo vigogo waliomshika mikono wakati anashugulikia skandali ya EPA, ESCROW na nyinginezo.
Mtakumbuka kwamba kuna kada mmoja wa ngazi ya juu anayetajwatajwa sana kuhusika katika biashara haramu ya meno ya tembo ambaye meno hayo yalipatikana yamepakiwa kwenye meli yake siku za nyuma yakiwa yamesafirishwa hadi nchi za mbali.
MAONI YANGU
Magufuli jiandae kwenda mbali zaidi kushughulikia waliotoa vimemo, kwa muktadha huo utakuwa umeiteketeza CCM nzima kuanzia juu mpaka chini.
Source:Jamii Forums
Aliyekuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dr Edward Hosea, Kutema Cheche
7
December 19, 2015
Tags
Wapambanapo mafahari wawili ziumziapo ni nyasi tu
ReplyDeleteyataje yataje baba
ReplyDeletewataje kabisa
DeleteMsoga hiyo
ReplyDeleteWatu watakufa kwa presha
wataje baba tuondoe mfumo na makundi
ReplyDeletetujenge ccm mpya
kwa manufaa ya watanzania wote
Kama wasingemfukuza angenyamaza milele?? TINGATINGA limeona mbali, hebu wafukuzwe wengine tupate 'maneno'........kwa sasa Tanzania inogile.......
ReplyDeleteVi memo
ReplyDeletePitisha mzigo huo
Lakini nawe Hosea unafanya kazi kwa vi memo
Basi hufai
Kumbuka ulivyokuwa ughaibuni ulivyokuwa ukiwanda mabosi wako
Tena kwa watu wadogo
Kueeleza Siri zao Na magonjwa Yao