Anachofanya Waziri Mkuu, Sio Sawa, Sio haki, Sio Good Governance...Ni Udhalilishaji na Kuaibishana!

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.

By Pasco-Jamii forums

Nafasi za Kazi

Post a Comment

33 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mjinga wewe na comments zako pumbavu mkubwa. Na wewe ni mmoja wa hao wanaoibia serikali yetu ndio maana unaongea hovyo kama vile umetapikwa. Wanaiba mchana kweupe na kumiliki mali kinyume cha sheria wakati wananchi wanakufa na njaa... Wewe kaa pembeni HAPA KAZI TU..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ila kuna watu wana akili zilizoganda jamani.kunyonywa kooooooooooooote,kubanwa kooooooote mbavu tunakobanwa watu wa chini bado tu unaendeleza akili mgando..........nakusihi siku nyingine kabla hujapost UTUMBO HUUU uliza wenye upeo wa kuona mbali kama inastahili au lah....HAPA NATAMANI NIKAMUAMBIE HUYO MAJALIWA USO NA MACHO HAWA WENGINE WANAOTUNYONYA MAANA NAONA
      WANACHELEWA KUWAFIKIA......Mwendo wa kipara wanga wote wa TANZANIA.

      Delete
    2. Wewe vipi ndugu yangu...???Rais na huyo waziri ni watumishi wa watanzania. ..Sisi tunataka kuona kazi tuliyowatuma..Sasa awapeleke pembeni kuongea nao kwani mali ya serikali ni yao..wanataka kutuonyesha wazi jinsi kazi inavyoendelea..mambo ya kupelekana pembeni ndo ufisadi na rushwa..wao waliiba kisiri Mwenyezi Mungu Anawaumbua..haya matukio yote ni Mungu Tuuuu uu. .Kumbuka Wazalendo wamenyonywa kwa miaka mingi Mno.Eee Mungu IBARIKI Tanzania yetu na Watanzania..Tulindie hawa viongozi wetu na Uzidi kuwajenga katika nafsi zao Imani Upendo na wazidi kukuogopa..Aamin!!!!

      Delete
    3. Wewe vipi ndugu yangu...???Rais na huyo waziri ni watumishi wa watanzania. ..Sisi tunataka kuona kazi tuliyowatuma..Sasa awapeleke pembeni kuongea nao kwani mali ya serikali ni yao..wanataka kutuonyesha wazi jinsi kazi inavyoendelea..mambo ya kupelekana pembeni ndo ufisadi na rushwa..wao waliiba kisiri Mwenyezi Mungu Anawaumbua..haya matukio yote ni Mungu Tuuuu uu. .Kumbuka Wazalendo wamenyonywa kwa miaka mingi Mno.Eee Mungu IBARIKI Tanzania yetu na Watanzania..Tulindie hawa viongozi wetu na Uzidi kuwajenga katika nafsi zao Imani Upendo na wazidi kukuogopa..Aamin!!!!

      Delete
  2. Toa utumbo wewe ulieandika hii habari,nyie ndio mnataka akina pinda wanaocheka cheka,kama mfanyakazi unafanya kazi yako vizuri kwa nini uwe na wasiwasi waziri mkuu kuja ofisini kwako?

    ReplyDelete
  3. Alichofanya waziri mkuu kiko sawa kabsa...sababu gani unaulizwa kama kuna tatizo unasema hakuna na wakati unajua kuna tatizo huyo officer alikuwa anamlinda nani wakt mkuu wake kamuuliza ...angesema tu hapa waziri kuna tatizo hili na hili...huyo mwigine kaulizwa swali dogo tu hela umekopa kwa kazi fulan na umezetumia kwa kazi fulan nani akitoa idhini...kashidwa kusema bas jibu hapo nikwamba hawakulipa mishahara wamekula hela.........hiyo way anayotumia iko sawa kabsa 100%

    ReplyDelete
  4. Ww ndiyo populist. Kwenye mfumo wa utawla bora uwajibikaji ni swala la msingi. Ukweli na uwazi. Sasa tuwaulize hao waliokuwa dhamana waliwajibika ipasavyo? Je walikuwa wa kweli? Yako mengi yanafanyika nje ya panzia Halafu kwenye screen kubwa tunaona na kambiwa nchi maskini. Ifike wakati sasa Tuwe na ajenda moja ya kitaifa. Kutokomeza mafisadi. Mafisadi, rushwa ni adui mkubwa kuliko ujinga, u maskini, na maradhi. Ndiyo maana madhara yakuwa na taifa lenye mafisadi yameanza kuonekana ktk ubaguzi wa huduma za afya, elimu, na malazi. Mafisadi wamejijengea shule zao, hospitali zao, Vyuo vyao. Mkulima au mtu wa kipato cha chini akifurukuta tu kueleka mtoto kwenye hizo shule . Board ya shule utasikia in awaita wazazi. Na kwa kuwa wengi ni mafisada utasikia pandasha ada ili tu was iona uwezo wajiondoe. Kwa mtazamo wangu tulibakiwa na miaka nichache sana ya amani. Lkn kwa kasi ya magufuli, bado tutakuwa na amani ya kudumu. Nashauri tu ili taifa liwe moja tuboreshe huduma za watu wa kawaida. Na hao mafisadi wale kibano cha ukweli. Hatuwezi kuwa na amani wakati Kuna wezi wa Mali za nchi na Kuna watu wasiojiweza. Kumbukeni pia wenye pesa wanadharau, Wanaweza kufanya lolote na wanyanyasaji.

    ReplyDelete
  5. Huyu nae au na wewe ni mpigaji

    ReplyDelete
  6. big up mh waziri mkuu hapa kazi tu hakuna kuchekeana weka wazi wananchi tujue madudu

    ReplyDelete
  7. Wazir mkuu ndo msimamiz mkuu WA kaZ zote Za serikali Sasa Kwann asifanye ziara Za kushtukiza? Maofisin uadilifu haupo Tena kiongoz akija wanampa takwimu na detail fake ili wao waendele kupiga pesa Za ambazo ni watanzania wote, sion ubaya WA yy kwenda tayar na details zake ambazo zinasadifu na nisahihi.. Kitendo cha kuuliza huku anajua ukweli wote ni kupima uadilifu WA wafanya kazi Lakin bado Tena kwa mala ya pili hawakua na uadilifu kazin wakawa wamdanganya... Mpka hapo ts enough me nahisi body nzima ya TRA pamoja na bandarin ifutwe na wahusika waachishwe kazi huku wakisubir kujib mashtaka yao.. Body zijengwe upya na watu Makin na sio Hao wapiga deal... Enough z enough Tanzania niya wote Kwann wengine wapige pesa zetu in extravagantly way? Sio fair watu wanamaisha magumu Sana kisa watu wachache Kwann iwe ivo? Hawa watu wametubetray watanzania wenzao na haki lazima ipatikane juu yao

    ReplyDelete
  8. Mtoa Mada sidhani kama anajitambua kwanamna moja au nyingine naona hata wewe unataka ziara ya kushitukiza.

    ReplyDelete
  9. Ktk mikundu we ni mkugunesi mtoa mada hivi we una akili timamu au znabebewa kwenye mfuko wa lambo? Mwizi aibe mchana kweupe akishikwa uanze kusema anadhalilishwaaa yeye alivyokuwa anaiba akujua anawadhalilisha wananchi wa kipato cha chini wanakosa sehemu ya kulala watoto wanashindwa kusoma huo siyo udhalilishaji bali udhalilishaji uliona ni kuojiwa hao majizi? Umenikasilisha ungekuwa karibu yangu ningekupiga sana mkunduuuuuuuuuu we na ukome

    ReplyDelete
  10. Jamani kwa haraka tu!!!!!mtoa mada ndo wale wale kama unafanya kazi vizuri kwa nn uwe na mashaka hata kama ukishtukiziwa??? mwenyewe umejitahidi kuandika upuuzi wako ukidhania utatu convince wa Tz, wewe naoana dose ya wagonjwa wa akili imekwisha wahi mirembe la sivy tutakukuta barabarani unaokokta makopo. Mungu mlinde Raisi wetu na watenda kazi wake wote walio na uchungu na Taifa letu TANZANIA, adui zao wakawe ni adui zako na vita yao ukawapiganie wewe mwenyewe atakaye wagusa awe amegusa mboni ya jicho lako.Amina

    ReplyDelete
  11. Kamkune mkeo na ma tx wako. Hujajiheshimu unataka akuheshimu nani?

    ReplyDelete
  12. Nadhani mtoa mada atakuwa amejifunza kitu tena usiamshe hasira za Watanzania waliolala wamechoka kwa umaskini. Ukiangalia comments zote zinakupinga wewe ndio ujue Tanzania ilipofikia sasa siyo tuliyokuwa tukiitaka tuna majonzi mengi katika mioyo yetu lakin sasa ni wakati wa Mungu ndio maana amesikia kilio chetu Watanzania. Nampongeza Rais na Waziri mkuu wake watu wawili kama jeshi lakin wanapiga kazi hadi tumesahau kama hatuna Baraza la Mawaziri Mungu awasimamie, Tanzania mpya inakuja tutanyoo tu.

    ReplyDelete
  13. hii ni nchi iliuojaa ufisadi na uhujumi uchumi na rushwa zisizo na mpango wwe muandishi kama unamwita mkeo na kumbembeleza hayo ni maisha yako hawa watu ni wezi wa siku yingi kwa nini waitwe ofisini ni haki ya kudhalilishwa mbele za watu watie adabu na walipe kwa wizi waliofanya

    ReplyDelete
  14. ww jamaa think before talk na wazungu wanasema no research no right to speak for me naona waziri mkuu yuko sahihi kabisa nchi yetu kwa ss inahitaji ukweli na uwazi habari za kuitana pembeni zilishapitwa na ndio chanzo cha rushwa huu ni mda wa kazi tuu no maneno anymore







    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba udaku HIZO COMMENTS M-FORWADIE WAZIRI..MAANA ZIKO JUUU..INAONYESHA WATZ WAMEKUNWA NA SHUTUKIZAJI YA WAZIDI MKUU..HIZO COMMENTS ZITAMSAIDIA AZIDI KUSHTUKIZA..NA kwa TAARIFA YAKO BIRA KUSHTUKIZA ASINGEFANIKISHA HILI JAMBO..SHUKRAN WAZIRI..ALLAH AKUTANGULIE..MAFISADI WOTE WALAANIWE

      Delete
  15. MFUMO WA UTAWALA NCHNI MWETU KWA SERIKALI HII YA AWAMU YA TANO CHINI YA RAIS MHESHIMIWA MAUFULI,NDIO MFUMO SAHIHI.MAGUFULI AMERITHI SERIKALI ILIYOWAKUMBATIA,KUWALINDA NA KUWASAIDIA WEZI NA WAHUJUMU UCHUMI.KESHATUAMBIA MHESHIMIWA HIVI KARIBUNI ATAPELEKA BUNGENI MAREKEBISHO YA SHERIA NA KUIBUA NYINGINE MPYA HUSUSANI MATUMIZI MABAYA YA OFISI,UFUJAJI MALI YA UMMA,UHUJUMU UCHUMI ILI WALE WOOTE WALIOHARIBU SIKU ZA NYUMA WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA KUTAIFISHA MALI ZOTE ZINAZOTOKANA NA KUIIBIA SERIKALI NA WANANCHI.TUPO PAMOJA NA MAGUFULI ASILIMIA 100%.AMA KUHUSU STAILI YA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA WA MHE.WAZIRI MKUU MAJALIWA TUNASEMA,KWA HALI TULIYONAYO HIYO NDIYO DAWA YA PEKEE KWA WEZI HAWA WASIO NA AIBU,WOGA WALA HURUMA KWA WATANZANIA WENZAO,KWANZA BADO HAITSHI,WASWEKWE LUPANGO.

    ReplyDelete
  16. Dawa ya moto ni moto. Waliiba gizani, wanakamatwa kweupeeeeeeeeeee! HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  17. mtoa mada lazima uwe na uzalendo wa nchi yako,kwanza nchi hii watendaji wengi wa serikali si wazalendo bali wanajari maslahi binafsi hivyo basi imefika wakati nchi inabidi iendeshwe kwa style ya kushitukizana kama ishara ya kubadili khali ya utendaji serikalini ambapo kwa muda mrefu watendaji walifanya kazi kwa mazoea na urasimu uliopitiliza ivyo basi unavyozungumzia mfumo wa utawala bora uadilifu ni kitu kimojawapo kilichopo ktk mfumo wa utawala bora je kama wanaiba mali ya uma kuna aja ya kuanza kuitana nyuma ya pazia huku wanakiuka kufanya kazi ktk misingi inayojali mfumo na maadili ya kazi.......anavyofanya waziri mkuu ni sahihi kabisa kwa masilahi mapana ya taifa letu.

    ReplyDelete
  18. Lakini jamani Mtu mzima ovyo
    Kwa mvi ugonjwa
    Umri na Picha mbona haviendani
    Au ndo ushauri WA binam da Slama

    ReplyDelete
  19. Angeanza kwa shemeji yake Msoga
    Kwani uzo wote huu umetokana na shemeji
    Pumbavu huyu mvaa wigi au kutia nywele rangi nyeusi
    Mtu mzima ovyo
    Inawezekana Kabisa chakula cha bwana kwanini usikubali natural yako nawe u Mtu mzima

    ReplyDelete
  20. Huyu mtoa mada ni mmoja wa waliomia ktk mchakato huu. TZ kuoneana aibu ndiyo kunatuangusha kwani ulipoajiriwa ulinambia ni siri? Unaujua serikali ni nani? Wananchi Na vipi uwahudumie kwa siri waliyekupa kazi? Uwazi. Ndiyo dawa ya wazembe kazini

    ReplyDelete
  21. naona hata baraza la mawaziri halina haja, makatibu wakuu wanatosha, ili kubana matumizi, mawaziri watafanya nini, sasa hivi kazi zinakwenda vizuri, wao ni ofa za kisiasa na wakati mwengine kupelekea matumizi yasio na ulazima, uwajibikaji hauhitaji mpaka uje ukaguliwe, kushindwa kujibu hoja auu kuficha ukweli ni kufeli ktk utendaji.

    ReplyDelete
  22. Huyu mtoa mada nadhani ni mfuasi wa mafisadi, hivi hata huyo mmkeo ungekuwa na ushahidi wa kutosha kwamba ametoka na jirani yako kimapenzi hivi ungerudi nyumbani na zawadi za kutosha na ukamuandalia yeye chakula then ukamuuliza pembeni because you have good governance? Mhe Waziri mkuu aliwapa nafasi ya kujieleza ili ajue kama kuna tatizo katika utekelezaji wa mifumo iliyowekwa ya kiutendaji but ile mizoba ika prove kwamba mifumo ipo sawa sawa so makosa yalikuwa ya wao watumishi na akili zao za kifisadi nazile fikra zao za kuona vyeo vyao ndo ni permit ya kufanya Watanzania wote Mafala kama mtoa mada , hata angelikuwa nani asingekuwa na patience kiasi hicho ulichokitaka Mhe. Majaliwa awe nacho, hivi huyo mkea akudanganye mbele za watu ww utamtafutia faragha kama unavyojidai? Hapa kazi tu! Huwezi kutekeleza majukumu yako bila rushwa, huwezi kuishi kwa kutegemea mshahara, Hakuna sababu ya kutaka utumishi wa umma, na bado.

    ReplyDelete
  23. Mtoa mada u cannot b serious, wacha wavune walichopanda yaani mtu mmoja Ana nyumba 80! damn.

    ReplyDelete
  24. HUYU MTOA MADA. NI MTOTO WA MWIZI. NDIO WALIKULA PESA ZA SERIKANI, SASA ANA TAPA TAPA MWAMBIE HUYO BABA YAKO ARUDISHE PESA . PU.................VU

    ReplyDelete
  25. Mtoa mada shame on you.......hii sasa ndiyo serikali ya watu, iliyowekwa madarakani na Mungu ili iwatumikie watu......enzi za kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu zimepita.....enzi za akili ndogo kutawala akili kubwa zimepita....sasa hivi akili kubwa inatawala akili kubwa.....lazima matokeo yonekane...big up Majaliwa.

    ReplyDelete
  26. Ulichokuwa unakitaka umekipata , kwani mtu akikuuliza kuwa wizi wao ni good governance autasemaje? acha ukuwadi wa siasa uchwara zitakuletea shida. Surprise kwa wezi kama hao ndiyo nzuri, na kwa bahati mbaya wamekuwa wakitumia fedha za wananchi na umma wa watanzania kwa kuongeza nyumba ndogo na wanawake vidumu na kujenga majumba ya kupangisha kana kwamba fedha hizo hazikuwa na wenyewe. Hivi wewe unalala gholofani na chumba cha mbwa wako kimewekewa viyoyozi uoni kuwa kufuru, ndugu yangu kwa ufisadi huo watanzania wangapi wamekufa kwa kukosa dawa na tiba sahihi? je ni wanafunzi wangapi wamefia madarasani kwa kuhangukiwa na kuta za shula ambazo si salama? walimu ni muda kiasi gani hadi leo wanaendelea kudai huku watu waiendekeza sherehe na makongamano? wewe umepewa ngapi ukilinganisha na fedha walizokwapua wao. Acha ujinga maana wewe uenda siyo mtanzania nadiyo mlikuwa mmefundishwa na maadui wa nchi hii kudumaza uchumi wetu na hatimaye kutuletea mauaji ya wenyewe kwa wenyewe. Mungu amepisha mbali shetani kateketezwa kwa moto wa shaba na gesi.ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete
  27. Mtoa mada vipi bado Una la kuongeza? Jibu unalo😅😅 shwain

    ReplyDelete
  28. stupid unataka kila siku wadhalilishwe wananchi wa chini sasa kosa ni lipi hapo kama wanataka heshima wafanye kazi wataheshimiwa, wanataka heshima ya kufichiwa madhambi kweli na wewe bado haujakua kiakili yawezekana na wewe ni mmoja wao na stay tune rungu laja

    ReplyDelete
  29. Usiwe mpuuzi kwa kuteletea habari za nyumbani kwako kwenye issues za taifa, kama ni udhalilishaji wameuanza wao kwa kutuibia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad