Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam na Mji wa Babati, Manyara Mhandisi Natty amefunguka.
Mhandisi Natty, aliyesimamishwa kazi jana kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili huko Kinondoni, amenidokeza kuwa anajiamini na hausiki kwa lolote. Mhandisi Natty amesema hiyo ni nafasi ya watanzania kujua kilichotokea Kinondoni.
'Najiamini. Mambo ya ukweli yatawekwa hadharani. Manispaa ya Kinondoni itatikisika. Ngoja niende nikawasikilize Wakuu wa nchi walioniamuru kwenda Dar es Salaam kusubiri uchunguzi juu ya tuhuma zangu' alisema Mhandisi huyo aliyehudumu katika Manispaa ya Kinondoni kwa muda wa kutosha.
Kuhusu kushughulikiwa yeye na kuachwa wengine kama Mkuu wa Wilaya na kadhalika, Mhandisi Natty alijibu: 'No comment'. Mchezo ndiyo kwanza umeanza. Vuta kiti ukae. Utazame hadi uzame. Usipepese macho wala kutikisa masikio!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Manyara)
CCM hiyo
ReplyDeleteMagufuli utafunga wengi
Kamati kuu CCM Chonde Chonde hatutaki kila kukicha kikao cha dharura kumpoza rais wetu mwacheni afanye kazi mwaka huu kazi
Si CCM si UKAWA sote kazi
Majizi, mafisadi mtaisoma namba
Mh waziri husika ONYESHA UADILIFU WAKO KATIKA HILO SUALA LA Ndg Natty.
ReplyDeleteNATTY MWIZI MKUBWA,KIBARAKA WA KUTUMWA,HAKUITIKISA KINONDONI WAKATI ANANEEMEKA LEO ANAGEUZA KIBAO KWA SABABU AMEFUKUZWA KAZI NANI ATAMSIKILIZA.HEBU AFIKISHWE MAHAKAMANI HARAKA MLA RUSHWA MKUBWA.
ReplyDelete