Ben Pol Ampigia Magoti Alikiba, Wayamaliza, Huenda Wakafanya Collabo

Wagombanao ndio wapatanao. Baada ya wiki nzima ya kuoga matusi kutoka kwa mashabiki wa Alikiba kutokana na kauli yake ya utata kwenye Twitter, Ben Pol amekiri kuwa aliteleza na kumuomba radhi muimbaji huyo wa Nagharamia.

Akiongea kwa simu kupitia kipindi cha Jahazi cha Clouds FM Alhamis hii ambako Kiba alikuwepo studio, Ben Pol alisema yeye ni shabiki mkubwa wa Kiba na anamchukulia kama kaka yake na amekiri kuwa tweet ile haikuwa sawa.

Mimi shabiki wa Kiba, moyoni mwangu nina furaha kubwa kuona kwamba tuko sawa kwa sasa,” alisema Ben ambaye aliimba wimbo ‘Njiwa’ wwa muimbaji huyo wakati wa mahojiano hayo.

Kwa upande wa Alikiba, alisema alishamsamehe muimbaji huyo wa ‘Ningefanyeje’ kitambo.

Ben Pol mimi bana kiukweli nilikuwa nimekusamehe toka nilivyokuwa nimeona ile lakini kwasababu nilishtushwa kama watu wengine walivyoshtuka nikajua labda utakuwa umeghafilika, lakini kiukweli mimi nilishtuka nilivyoona vile,” alisema Kiba.

Najua ulikosea ndio maana nikaona basi yaishe kwasababu binadamu tunakuwaga na makosa hayo.”

Ben Pol alimalizia kwa kusema, “Mwenyezi Mungu anakuwga na mipango yake, hatuwezi jua, pengine hapo mbele kunaweza kuwa na bonge ya collabo.”

UNAHISI COLLABO YA ALIKIBA NA BENPOL ITAKUWA MOTO?


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad