Breaking News: Godbless Lema Aibuka Kidedea, Afanikiwa kutetea Jimbo lake la Ubunge Arusha


Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godblees Lema ameibuka Mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.

Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya Siasa Mh Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM Bw Philemon Mollel aliyepata kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.

Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Pamoja na Navo Mollel wa ACT Maendeleo aliyepata Kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi Mwinyi wa CUF aliyepata kura 106. Sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa NRA aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bw Juma Iddy, jimbo la Arusha wapiga kura walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hilo tulitegemea, chadema ni ya kanda kaskazini, hata JPJM alipata kura chache katika kanda hiyo, hivyo hatushangai sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. aliyekuambia unatakiwa kushangaa ninani? wewe inabidi ukubali tu, mijini hamna ngome nyie, kwenu vijijini!! kwa wachache walio elimika!

      Delete
  2. alipata kura za kihalali nyingi wapi nchini,wezi wakubwa,mijizi.lema ni chaguo la watu wa arusha.labda niwakumbushe.jimbo la arusha mjini kama jiji lina madiwani 34.kati ya hao 33 ni wa ukawa-chadema na mmoja[1] ni wa ccm.nikuchekeshe kwenye kugombea UMEYA ARUSHA HUYU WA CCM ALIJAZA FOMU WAKIUTAKA UMEYA,KURA MATOKEO: UKAWA CHADEMA 33,CCM 1.AIBU,AIBU,WIVU,KUKOSA AKILI,DHAMIRA YA FUJO,UKO PEKE YAKO WENZIO 33,KWA NINI USIAMUE ANGALAU KUKAA KIMYA?

    ReplyDelete
  3. Jembe limerudi mjengoni

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad