Kigogo mmoja mzito wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) amezuiwa kusafiri kwenda nje ya nchi yeyey na familia yake kutokana na zuio lilipo kwa sasa kwa watumishi wote wa umma.
Kigogo huyo alikutwa na songombingo hilo baada ya kufika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA)kwa minajiri ya kwenda nje ya nchi kwenda kula bata na familia yake wakati huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka (Xmass na mwaka mpya). Kigogo alidai kuwa safari hiyo alikuwa kagaramikia yeye
mwenyewe kwa pesa yake , wala siyo ya serikali, ila waksema kuwa kwa sasa kuna pini ya kwenda nje
ya nchi kwa mtumishi wa umma .
Kigogo huyo alihojiwa katika chumba maalumu na maofisa wa uhamiaji kwa muda wa kutosha lakini majibu yake yalionekana kujikanganya na kukosa msingi, hivyo aliamrishwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha hapo uwanjani kabla ya kutumbuliwa jipu kama wale wanne wa TAKUKURU walivyotumbuliwa.
Source: Citizen
Breaking News: Kigogo wa BOT Azuiwa Airport Kutokana na Kukosa Vibali vya Kusafiri nje ya Nchi
7
December 17, 2015
Tags
hii habari imekaa kidaku daku
ReplyDeleterais kazuia safari za kikazi zisizokuwa na ulazima
sasa huyu anasafiri kimpango wake na familia yake
mgemtaja basi huyo kigogo
hii habari ya uzushii
pini hiyo, alikuwa anakimbia nchi huyo akijua yeye ni jipu lijalo!
ReplyDeleteKama kwa pesa yake kwanini atoloke wasijue asipoelekea angekaa asubiri sheria fisadi uyooo
ReplyDeleteWanakimbilia nje kuweka mambo sawa katika account zao za nje. Hakuna kutoka mtu mpaka tupate repoti ya account zenu huko nje. JPJM alisema wametuibia kiasi cha kutosha, wametuchakachua kiasi cha kutosha, SASA BASI, NA BASI KWELI.
ReplyDeleteMlisema mpo tayari kwa mabadiliko, hakuna kuishi kwa mazoea........HAPA KAZI TU
Tuwe waangalifu na maamuzi mengine
ReplyDeleteWatendaji msiige kila kitu
Fanyeni kazi kwa ungalifu
Yasije token kama samaki wa Magufuli
Hii sasa ishakuwa kuwa shida labda ana marafiki zake au ndugu tuuishio ughaibuni
ReplyDeleteTusinyanyasane kiasi kwa kulipiza kisasi
Samaki WA mafuguli walitocost meli ilikaa miaka uliza kiasi gani tulilipa mbona hamsemi
Magufuli kasema Safari za kikazi hata kama zimeghalimiwa na wafadili lazima Kibali toka ikulu, Kama ni kuzuia hata kikwete basi mzuueni tujuwe nani kalipa gharama za Safari hii pamoja Na walinzi wake
labda alikuwa anatoroka kijanja!!
ReplyDelete