Breaking News: Mapema Asubuhi ya Leo Dkt. Hamisi Kingwangalla Atumbua Majibu ya Watumishi Wachelewaji Wizara ya Afya

IMG_9118
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, akiwaamrisha askari wa getini wizarani hapo kuweka kufuli na kutoruhusu mtumishi yoyote wa ofisi hiyo kuingia ndani ya ofisi za wizara ilipotimu saa 1:32 asubuhi mapema leo.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_9122
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akisimamia zoezi la ufungwaji wa geti hilo, Kulia ni askari wa SUMA JKT akiweka kufuli katika lango kuu la kuingia katika ofisi za Wizara ya Afya.
IMG_9123
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiwauliza askari wa getini kuhusu daftari la mahudhurio ya watumishi wa wizara baada ya kufungwa geti hilo, na kupewa maelezo kuwa watumishi huonyesha vitambulisho pekee na husaini katika vitengo vyao.
IMG_9139
Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Afya akiwasili ofisini huku muda wa kuingia kazini ukiwa umepitiliza. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na mmoja watumishi wa wizara hiyo na kuagiza kuletewa vitabu vya mahudhurio kwa vitengo vyote vilivyopo wizarani hapo.
IMG_9149
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Afya, Michael John akitoa maelezo kuhusu mahudhurio ya watumishi kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.
IMG_9155
Magari ya watumishi wa Wizara ya Afya yakiendelea kuwasili ofisini bila ya kutambua kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri, Dkt. Kigwangalla ametoa agizo la kuizuia watumishi wachelewaji.
IMG_9156
Askari wa getini wakimpa maelezo mmoja wa watumishi wa wizara hiyo kuwa Mh. Naibu Waziri ameagiza watumishi wote waliochelewa kuzuiliwa kuingia ndani.
IMG_9164
Mmoja wa wasaidi wa idara ya rasilimali watu akimkabidhi vitabu vya mahudhurio Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.
IMG_9172
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitia mahudhurio ya watumishi wa wizara kwa siku zilizopita.
IMG_9181
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitisha mstari wa kufunga mahudhurio kwa watumishi ambao wameripiti kabla ya saa 1:30 asubuhi ya leo.
IMG_9198
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiendelea na zoezi hilo la kupitisha mstari kwa kila idara za wizara hiyo.
IMG_9231
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu juu ukaguzi huo katika ofisi za wizara yake ya afya ili kuboresha utendaji wa wizara hiyo na vituo vyote vya sekta ya afya nchini kote.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnalalamikia foleni za magari na barabara hazitoshi na kila siku mnanunua magari kwa kushindana kama hamna akili nzuri vile na kusahau kuwa slowly slowly but sure mnayaharibu mazingira kwa pullution vumbi jingi sana hapo Dar watu mnaona ni kawaida tu matokeo yake ni magonjwa ya ajabu ajabu yanayosababishwa na moshi uliotumika kutoka katika magari yenu yasiyozimwa engine hata foleni iwe ya masaa kadhaaa magari yenu engine ipo on tu mnai pollute Dar daily people wake up!!!Thinking you're living in paradise but you're living in your own hell time will tell

    ReplyDelete
  2. Hii sasa sifa
    Tatizo ni usafiri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao walowahi wamefikaje? Ndio mlivyo wafanyakazi wote wa serikali, mnafika muda muutakao, ukiwa na shida na mtu utasubiri mpaka basi, akishaingia wala hajali kama kuna watu wanamsubiri, atatoka kwenda kunywa chai mpaka saa 4 ndio anaanza kazi.....TUMEWACHOKA. aKigwangwala KIMBIZA HAOO

      Delete
  3. Safi sana mhe. waziri..... kaza buti kaka yetu mpendwa na Mwenyezi Mungu akutangulie daima. jamani kufanya kazi ktk ofisi za serikali imeshakua mazoea mabaya sana humjui bosi nani mdogo nani yani ni kama familia ya kambale wote wana ndevu kuanzia bosi hadi mfagiaji mtu anaingia ofisini kwa muda anaoona yeye kua unamfaa. hatuna hata hofu ya Mungu kwa wale tunaowahudumia jamani.. Mhe. Raisi tuletee waziri wa Elimu fasta na huku nako watu wapo tu kwa mazoea.

    ReplyDelete
  4. hahahaaaa..... ni pale baba anapowahi kufika nyumbani na kufunga gate wakati watoto bado wapo nje wanakula good time. chapa viboko wote!!!!

    ReplyDelete
  5. kama wizarani kwenyewe ni hivi pata picha kwenye ofisi zingine ambapo mawaziri wala makatibu hawajawahi hata kupita kwa nje tu hali ikoje?? ni uozo, na uvundo mtupu.

    ReplyDelete
  6. Mahospitalini nako wauguzi wanaroho mbaya

    ReplyDelete
  7. Amechelewesha kitu kimoja mh. angechapa viboko kama yule mkuu wa wilaya aliyewahi kuchapa waalimu baadaye wakamlazimisha ahame. sasa kwa wakati huu hatahamishwa maana atakuwa anatimiza dhana ya hapa kazi tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad