BREAKING NEWS: Waziri Mkuu Majaliwa Atinga Tena Bandarini...Angundua Upotevu wa Makontena Mengine 2431

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amefanya tena ziara ya kushtukiza bandarini na shirika la reli Tanzania(TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini.

Katika maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.

Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.

Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.owote !!

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naona hawa watu huko bandarini na hao TRA ni magombe sugu kwa wizi. Hao watu na kiongozi wetu aliyemaliza muda wake. Wangeingamiza kabisa hii nchi. Ingefutika kabisa kwenye ramani ya ulimwengu kwa ugombesugu wao

    ReplyDelete
  2. Naona hawa watu huko bandarini na hao TRA ni magombe sugu kwa wizi. Hao watu na kiongozi wetu aliyemaliza muda wake. Wangeingamiza kabisa hii nchi. Ingefutika kabisa kwenye ramani ya ulimwengu kwa ugombesugu wao

    ReplyDelete
  3. Wafanyakazi wa Bandarini wengi wao wamejenga majumba kutumia majina ya ndugu zao, pia nao wachunguzwe hao ndugu wamepata wapi pesa????.

    ReplyDelete
  4. sina cha kusema nakaa kimya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad