Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya Escrow.
Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Handeni, akimnadi Daudi Lusewa.
Alisema baadhi ya mawaziri, akiwamo Muhongo, bado hawajasafishwa na tuhuma za rushwa zilizosababisha wajiuzulu hivyo wajiandae kwani wabunge wa chama hicho wamejiandaa kumwangusha.
Mnyika alisema amemshangaa kuona Rais John Magufuli akimteua Muhongo kwenye Wizara ile ile alikopatia kashfa, iliyosababisha Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumtema kwenye Baraza la Mawaziri.
“Hatukubaliani na uteuzi wa Profesa Muhongo na namhakikishia bungeni patachimbika,” alisema Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba, Dar es salaam.
“Hoja yetu ya kwanza tutakapoingia bungeni tu itakuwa kushinikiza Waziri huyu ajiuzulu maana bado hajasafishwa,” alisema Mnyika.
Chadema Bado Hawajakubali Yaishe...Waapa Kumshughulikia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Bungeni
6
December 14, 2015
Tags
Hivi Lowasa mlimsafisha vile??
ReplyDeleteMnyika, sio lazima uongee, kama huna la kusema ni bora unyamaze, cdm mlizunguka nchi nzima na hilo FISADI NYANGUMI lenu mkiliombea kura, huku mkijua fika kwamba ni 'chafu'. Jiandaeni'kususa' na 'kutoka' bungeni kama kawaida yenu, lakini sio kumshungulikia Muhongo, jeuri hiyo HAMNA!!! MSHAISOMA NAMBA
ReplyDeletemagufuli kajiharibia sana kumteua huyu muhongo
ReplyDeletenilichosikia katika pitapita wanadai huyo muhongo ndo msomi pekee wa hiyo idara ndo maana hawana jinsi so usishangae wanavyomtetea amewazidi usomi... sijui akifa watafanyaje.. nchi imejaa wasomi vilaza msomi wa ukweli ni mmoja tu pro muhongo ndo maana hatujali ufisadi wake.
ReplyDeleteHuyu muongo sijui mohongo
ReplyDeletekujiuzuru
Alilazimishwa kujiuzuru
Tena kwambinde
Tena ana mdomo mchafu dharau ya kimsoma
Kama kweli msomi angekaa huko huko ulaya
Hana mpango wowote
Mwizi tu huyu tunaye bungeni
kazi kwanza ngonjera badae.tutafuteni namna ya kuwasaidia wananchi sio kujadiri yalopita
ReplyDelete