CHADEMA kumleta Lowassa ni Sawa Kujichimbia Kaburi la Kisiasa

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ule utabiri wetu kwamba iwapo Wana CHADEMA wataendelea kutii matakwa ya viongozi wao kwa staili ya ndio mzee itawazamisha wao na CHADEMA kwa ujumla sasa unaelekea kutumia.

Laiti wana CHADEMA wangejenga utamaduni wa kuhoji kila uamuzi unaofanywa na viongozi wao, wakapinga au kukubali maamuzi hayo baada ya mijadala ya kina haya yasingetokea.

Kitendo cha CHADEMA kumkaribisha Waziri mkuu mstaafu mh Edward Lowassa kumechafua hali ya hewa ya kisiasa ndani ya chama.

Nakumbuka maneno aliyowahi kuyatamka Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA Dr Slaa kwamba kitendo cha CHADEMA kumleta Edward Lowassa ndani ya chama ni sawa na kuchota kinyesi na kukihamishia chumbani, hii haimaanishi kwamba Lowassa mwenyewe ni mchafu (fisadi) ila msururu wa marafiki zake wenye kashfa lukuki za ufisadi ndio wangekichafua chama.

Habari za kuibuliwa kwa tuhuma za watu walioshiriki katika kashfa ya fedha zilizoibiwa za Stanbick huku vinara wa skendo hizo wakiwa ni watu wa karibu wa Lowassa inazidi kuibua maswali mengi kuhusu uadilifu wa Eddo.

Mpende msipende wana CHADEMA kwa umoja wenu mmeamua kufanya uamuzi mbaya wa kukizika chama, CHADEMA wamepoteza mwelekeo,tangu wamlete Lowassa neno UFISADI limekuwa msamiati mchungu midomoni mwa CHADEMA, hawaongelei tena ufisadi.

Si Lowassa wala Mbowe aliyejitokeza kusifia jitihada za rais Magufuli katika kupambana na wahujumu uchumi nchini, si jambo la kustaahabu kutoka kwao kwasababu hata wakati wa kampeni hawakutaka kabisa kuongelea ufisadi.

Katika wakati huu ambao kashfa mbalimbali za ufisadi zinaibuliwa,wahusika wengi wanaotajwa ni watu wa Lowasaa na wengine walikuwepo katika timu ya kimkakati ya kampeni ya Lowassa.

Lile kundi la watu wenye kashfa lukuki za ufisadi sasa limehamia CHADEMA, bila kutarajia CHADEMA wamegeuka kuwa CCM ya miaka 2005 hadi 2015 ambapo ilikuwa ikiandamwa na ufisadi.

CHADEMA wamechukua kijiti sasa, sasa wajiandae kupokea mashambulizi makali kutoka kwa akina Nape bungeni, mkijaribu kuikosoa CCM watawakumbushia kuhusu Eddo na kundi lake mliowapokea huko CHADEMA.

Kwa kifupi,CHADEMA mmepoteza moral authority ya kuikosoa CCM kwa jambo lolote lile maana mmeamua kuyafanya yale yale mliyokuwa mkiwapigia kelele CCM.

By TEKNOLOJIA-Jamii Forums


Nafasi za Ajira Kutoka Magazetini

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nape katika watu wapumbavu na wajinga
    Hakuna shule ya kuunga unga
    Huyo abakie huko huko CCM
    Bungeni hakuna taarabu , kuna hoja na kujua kanuni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aende kuimba taraabu na kopa huyu nape

      Delete
  2. Kweli kabisa mzee, ila mpaka yatakapowakuta hawataki kusikia kwa sababu ya Ukanda, ukabila na kupenda mteremko Eddo anatoa fedha nyingi amabazo hazima masli kwa chama ila kwa mtu mmoja mmoja.Kwa hali hii uenda wkapoteza heshima yao kwa kulazimishwa kuondoka na kuachia nafasi zao.Eddo na Freddy wamkaa miaka mingapi ccm na pm walipata halafu leo wanasema hakijafanyika kitu. Mimi nawaeleza kuwa walivyotoka ccm na ndivyo watakavyotoka Chadema kwa aibu na kudharauliwa hadi kaburini.ALUTA CONTINUA

    ReplyDelete
  3. Ndugu mwandishi,wananchi tunaposema kwamba ACT ndio tunakiona chama ambacho kinaweza kuikosoa CCM unadhani tunabwatuka tu?sio, tunamaanisha.
    CHADEMA(UKAWA)kwishnehi.Halafu wanachekesha hawa watu,kwa kujifariji wanasema eti yote anayofanya magufuli sasa hivi ndio ilikuwa sera zao,mbona hatujawahi kusikia wakikemea ufisadi kama Magufuli alivyokuwa anapiga kelele kwenye majukwa wakati wa kampeni,na kwa kuapa ya kwamba mafisadi atalala nao mbele,atafungua mahakama ya mafisadi nk?Magufuli anatufurahisha WaTZ mpaka basi.Na kwa imani yangu jinsi CHADEMA walivyo na tabia za kuzua na kuzusha mambo,kama Magufuli angekuwa kajilimbikizia mali wangekuwa wameshaanza kuleta ngebe,lakini hawana na hawajui waanzie wapi,Magufuli yuko safi hata kama ana doa basi ni kidogo sana.Mungu tunakuomba umlinde rais wetu.

    ReplyDelete
  4. Huyo Lowasa na Sumaye pamoja na babu yao Kingunge wametumwa na CCM kuja kuimaliza Chadema, hakika wamefanikiwa kwa asilimia 95.99% walijua Mbowe anatamaa ya pesa lazima angekubali huo mpango, na kweli DJ akaingia chaka, kabadilisha gia angani, CCM wanapeta, katika uchaguzi wa mwaka huu, laiti ukawa wangemsimamisha mtu tofauti na Edo, CCM ingepigwa chini maana watu walishaichoka, lakini wakimwangalia huyo mgombea mwenyewe wa ukawa na sifa zake mmmh, wakaona hapana bora ZIMWI LIKUJUALO....................... kuna mtu alimpigia simu DJ kumshauri msimchukua Edo atawaharibia chama, akibisha......kumbe SIKIO LA KUFA.................

    ReplyDelete
  5. Nyie endeleeni kujitekenya na kucheka wenyewe,CHADEMA itaendelea kuwepo na wala si ya mtu mmoja,cha muhimu pigeni kazini sababu ndio falsa ya ccm hapa kazi tu!walio mchagua lowasa wala siyo wanachama wa chadema,na chama chochote kinapokuwa madarakani kinatakiwa kifanye mambo muhimu kwa nchi la sivyo kitatolewa madarakani.

    ReplyDelete
  6. acheni kuweweseka ondoeni uvyama hapa kazi tu, kampeni zilishapita....ccm wenyewe hawamtaki magufuli..... magufuli wa wote.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad