CHADEMA Watoa Mpya...Wasema Magufuli Anatekeleza Sera za Wapinzani

Wakati Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli akionekana kuteka hisia za Watanzania wengi, Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  kimesema hakishtushwi kwani amekuwa akitumia  hoja, mikakati na Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, amesema kuwa wakati wa kampeni Chadema ilieleza jinsi ya kupambana na  ufisadi, kuwa na utaratibu bora wa utendaji kazi, uadilifu na uzembe wa watumishi wa umma, mambo ambayo sasa yanafanywa na Dk Magufuli.

Hata hivyo, alisema kwa kuwa anachofanya hakikuwamo katika mipango ya Chama cha Mapinduzi (CCM), anaamini atakumbana na changamoto siku zijazo.

 “Akiomba ushauri tutatoa kwa maana namna gani atekeleze, lakini ni mapema mno kusema kama ana dhamira ya kuyafanya. Pengine anayafanya kwa ajili ya kujitafutia umaarufu wa harakaharaka,” alisema Mwalimu.

Mikakati ya Dk Magufuli
Tangu Novemba 5 mpaka sasa, Dk Magufuli ametangaza mikakati kadhaa ya kubana matumizi ya Serikali, ili kuimarisha huduma za jamii, sambamba na kufichua na kuminya mianya ya rushwa na ufisadi.

Miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni kusitisha safari za nje, kupiga marufuku michango ya aina yoyote kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi kidato cha nne, kufuta sherehe za Uhuru zilizotajwa kufanyika Desemba 9 na kuagiza fedha za sherehe hizo zitumike kujenga barabara pamoja na kuibua madudu ya ukwepaji wa kodi la rushwa katika Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mwalimu alisema mambo hayo ni kati ya mengi yaliyokuwa yakipigiwa kelele na Chadema pamoja na vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kabla na wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25.

Mambo haya (yanayotekelezwa na Dk Magufuli) tulikuwa tumeyapeleka mbele ya Watanzania ili watuamini na tuwafanyie. Wananchi wanajua nini kilichotokea na si ajabu kuona wao (Serikali iliyopo madarakani) wanachukua ya kwetu na kuyafanyia kazi, maana Watanzania ndiyo walioyachagua na ndiyo waliyokuwa wakiyataka,” alisema.

Huku akitolea mfano hoja za Chadema za ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma (Udom) na kuandikwa kwa Katiba Mpya zilivyotekelezwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Mwalimu alisema: “Uungwana ni vitendo (Dk Magufuli) atakapokuwa anayafanya si vibaya akasema jamani haya yalikuwa si ya kwangu bali nimeyakopa kutoka kwa wenzangu.”

Alisema si vibaya kwa kiongozi au chama kuiga mambo mazuri ya chama kingine na kusisitiza kuwa lengo la upinzani ni kuona mambo ya msingi yanafanyika ili nchi iwe na maendeleo.

Suala atafanikiwa kwa kiwango gani hilo ni suala jingine, kama  anayafanya kwa utashi au kwa kuwahadaa Watanzania hilo ni suala jingine.

Mwishowe kama si lako linakuwa na changamoto katika kulitekeleza,” alieleza.

Alisema wapinzani hawawezi kuishiwa hoja za kuikosoa Serikali ambazo nyingi zinalalamikiwa na wananchi, “Mambo yetu mengi wameyachukua ila swali linakuja je, wanaweza kuyatekeleza? Chadema ni chama chenye ubunifu wa hali ya juu katika kutafuta suluhu ya kero za wananchi.”

Alisema chama hicho sambamba na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),  wataendelea kuumiza vichwa ili kutafuta jinsi ya kuzitatua kero zinazowakabili wananchi.

Tunachokitaka kukiona ni Watanzania wakipata haki zao na maendeleo, waishi  katika nchi yenye demokrasia, utawala bora na misingi mizuri ya sheria,” alisema Mwalimu.


Nafazi za Kazi Kutoka Magazetini

Tags

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hamna jipya bandugu.Kwanini kwenye kampeni hamkuwa mnapinga ufisadi?
    Ninachokiamini,CHADEMA mafisadi wako pia kama ilivyo CCM,tena mapapa kuliko,ndio maana kwenu ufisadi mlikuwa hamuukemei kwa kuwa ilikuwa ni sawa na mtu kujichapa fimbo mwenyewe.Na hakika Magufuli ana akili sana na aliona mbele na ndio maana alikuwa anamalizia neno YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO,hii inapendeza kusema kama kuwafunga mtafungwa wangapi?maana ni wengi,ni bora mafisadi waliobainika/watakaobainika walipe pesa,wataifishwe tugange yajayo.Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Wanafiki wakubwa nyie chadema,.......JPJM alikuwa akisema tangu wakati wa kampeni kwamba ataanzisha mahakama ya mafisadi na majizi ili yafungwe haraka, ni lini nyinyi mliyasema?? Kama kweli mnapiga vita ufisadi mbona mlimuazima Lowasa ambaye alitajwa kwenye orodha yenu ya mafisadi, agombee uraisi kupitia chadema?? Chadema ni wapinzani, na kazi yenu PEKEE mlonayo kwa sasa ni KUPINGA TU, hamna jipya......HAPA NI KAZI TU, UNAFIKI KWENU

    ReplyDelete
  3. HIVI TUSHIKE LIPI, JUZI ZITO KASEMA HIZO NI SERA ZA ACT, LEO CHADEMA WANASEMA NI SERA ZAO, TUNASUBIRI KESHO KUSIKIA VYAMA VINGINE VITASEMAJE...........!!!KAMA MNAMWONEA WIVU JP NI BORA KUUCHUNA, KULIKO KUJIDHALILISHA

    ReplyDelete
  4. Hahahahah chadema mnatuchekesha, msitufanya wa TZ ni wajinga kiasi hicho, wakati wa kampeni HAMKUTHUBUTU japo kugusia kuhusu UFISADI, mliona haya na aibu kwakuwa mlikuwa nalo FISADI PAPA jukwaani mnalipigia kampeni eti liwe raisi wa Tanzania (mmeshindwa na mmelegea)

    ReplyDelete
  5. Mmmh! Labda chadema ile ya mwanzoni ya Dr. Slaa, sio chadema hii ya sasa ya mzee wa kubadilishia gia angani aka 'mpigaji', mzee wa madili........mmeshauza chama, hamna jipya....HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  6. Na kweli hiyo ni MPYA na ndio maana ikasemwa na huyo kaimu katibu mkuu, alokosa haya na aibu, wala hajui alisemalo, hao 'vingunge' wake nafsi zao zinawasuta wakamsukumia yeye aseme.......chadema mmeishiwa, hamna kazi za kufanya sasa mmebaki kuropoka. basi hata hilo jina la John pia kaiga kwenu, na nyie pia si-mnaye John....mfyuuuuu WATUWAZIMA HOVYOOOO

    ReplyDelete
  7. Hivi ukawa wana ILANI YA UCHAGUZI??? Mnajidanganya wenyewe, mnajiona mnapoteana sasa mnatuletea viroja, hebu kwendeni zenu wanafiki wakubwa nyie....hatuwaelewi na hamtuambii kitu kwa JPJM, HAPA NI KAZI TU

    ReplyDelete
  8. Chadema mnamtaja taja Mh. Magufuli kama nani wenu??? nyinyi mlishasema hamumtambui na hamko tayari kufanya nae kazi, iweje leo mnakula matapishi yenu kama kawaida yenu kwa kusema eti akitaka ushauri mtatoa, NYINYI NI KAMA NANI??!!?? Hebu mwacheni JP afanye yake, endeleeni na msimamo wenu wa kutomtambua ili awe na amani ya moyo, MAGUFULI NI CHAGUO LA MUNGU.

    ReplyDelete
  9. MLIPO FANYA VITUKO BUNGENI MLIDHANI MTASIFIWA, BAADA YA KUONA WATU 'WAMEWAPOTEZEA' MNATAFUTA KICK KUPITIA MGONGO WA 'TINGATINGA'. MNAJISUMBUA BURE BURESHI, KWA KIFUPI HAMNA MVUTO.........JPJ MAGUFULI NDIO HABARI YA DUNIA KWA SASA....HAPA KAZI TU......

    ReplyDelete
  10. WAMEANZA KAMPENI MPAKA WAMEMALIZA HAWAJAWAHI KUONGELEA UFISADI LEO WANASEMA MAGUFULI ANATUMIA SERA ZAO . HUO NI ULOFA NA UPUMBAVU.

    ReplyDelete
  11. Hey people will you please stop these quack quack bullshits and let us all be ONE and try damn hard to build our lovely falling Nation instead?

    ReplyDelete
  12. Nyinyi wote mnaokanusha hapo juu mnaonrkana wazi hamna elimi za juu

    ReplyDelete
  13. MALOFA WATAISOMA NAMBA NDO KWAAAAAAAAANZA TINGATINGA LINACHANJA MBUGA

    ReplyDelete
  14. Na mfumo je mwalimu unadanganya nini kuhusu hili. Mlisema mfumo ndio mbaya. ukawa wote Ni ZUzu hamjitambui hata kidogo

    ReplyDelete
  15. masikini wana mihemko....wenyewe waliojilimbikizia mali wapo kimya wanakula kwa raha ona malofa wa fisiem na malofa wa ukiwa wanavyopata jazba na comment zao za kujiona wao ndo wakosahihi.

    ReplyDelete
  16. Mtasubiri miaka 1000 kutawala nchi hii... Mmekoa la kuongea sasa.. endeleeni na migomo yenu kama kawaida yenu. Tumewachoka!!!!

    ReplyDelete
  17. Chadema kaeni chini mjipange upya!
    Hilo fisadi papa lenu mlilolizoa huko fisiem limewameza wote mmekalia kulia tu!
    Kampeni zilishaisha na ninyi mmesema hamumtMbui rais sasa anatekelzaje sera zenu? Nyie si hamumtambui.
    Tutokeeni hapa,!
    CCM mbele kwa mbele!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad