Toka jana nimefutilia mijadala na kauli za Mnyika kuhusu kuhamishwa kwa TAMISEMI na leo tena kuibua inshu ya ESCROW.
Pia nimeendelea kuona matamko yanayofuatana tu kutoka kwa Tumaini Makene.Chama changu CHADEMA, staili tunayoitumia saiv tutachokwa sana mapema,tuache siasa za matukio tufuate siasa za hoja. Lipumba naye leo katupiga dongo, saiv tumekazania mambo ya Makonda...hayatatusaidia hayo, tunaomba tuendelee sera zetu za kuibua ufisadi.
Nashukuru Mnyika amesema ataibua hoja ya Escrow,ni vizuri sana ila naomba pia na Richmond irudishwe, Kubenea mpambanaji wangu naomba upeleke hoja binafsi kuhusu Richmond kamanda ili wahusika wawajibishwe..
ni kweli kabisa mtoa hoja, lakini Ufisadi huo uliotajwa hapo juu mmoja sidhani kama utaendelea kuibuliwa, ngoja tuendelee kusubiri tuone, Mungu atupe uzima.
ReplyDeleteThubutu yao, sio kwa chadema hii! Wataibuaje ufisadi wakati wao wenyewe wote hivisasa ni mafisadi, wapiga dili, hawana hoja, hawana jipya, wanasubiri mtu 'ajambe' wao wadandie juu-kwa-juu hatakama haliwahusu.... Iliwarudi kwenye line, chakufanya, wamrudishie Edo pesa zake zote alizonunulia chadema, waanze upya, kwa sasa hawana ujasiri wa'angalau kutamka neno FISADI huku wakijua lile FISADI KUU wamejaribu kuliombea urais, watu waka'mpipo pwa
ReplyDelete