Diamond Platnumz akiwasalimia mashabiki wake waliofurika katika eneo la Karume leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu shoo yake itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda sambamba na mashabiki waliofurika Karume leo.
Mashabiki wakiwa wamepagawa wakati Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Meneja Masoko wa Global Publishers na Dar Live, Innocent Mafuru (mwenye tisheti nyeupe aliyesimama kulia) akiwakaribisha wanahabari, wasanii na mashabiki wa burudani katika mkutano na wanahabari kuelekea shoo ya Funga Mwaka itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akielezea jinsi walivyojipanga kwa shoo hiyo ya Krismasi.
Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akionyesha kadi ya Airtel Money Tap Tap inayomuwezesha mteja kufanya malipo mahali popote na watakaohudhuria shoo ya Diamond kununua tiketi kwa punguzo la shilingi 5000 kwa wateja 1000 wa kwanza.
Mratibu wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akiongea na wanahabari pamoja na mashabiki (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuwapa burudani mashabiki siku ya Krismasi.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Staric ambaye naye atapanda jukwaani siku hiyo akiongea na mashabiki.
Diamond akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.
Baada ya kuongea na mashabiki wake Diamond aliamua kugawa CD na DVD za nyimbo zake kwa mashabiki waliohudhuria.
Diamond akiwaaga mashabiki na kuwataka wakutane Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi.
Mashabiki wakiwa wamemzingira Diamond wakati akiondoka eneo la mkutano na wanahabari leo.
kipenzi cha watu
ReplyDeletesafi sana mondi watasubiri sanaaaaaaaaaaaa
Kuna kundi fulani hawataki hata kusoma habari zake,ila ndio basi tena jamaa kafunika!
ReplyDelete