Diamond Afanya Kufuru Kariakoo Karume..Atoa Show ya Bure na Kusema "Njooni Dar Live Siku ya X-mas, Sitawaangusha"

Funga Mwaka Concert 2015 (7)Funga Mwaka Concert 2015 (9)
Diamond Platnumz akiwasalimia mashabiki wake waliofurika katika eneo la Karume leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu shoo yake itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (10)
Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda sambamba na mashabiki waliofurika Karume leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (8)
Mashabiki wakiwa wamepagawa wakati Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Funga Mwaka Concert 2015 (1)
Meneja Masoko wa Global Publishers na Dar Live, Innocent Mafuru (mwenye tisheti nyeupe aliyesimama kulia) akiwakaribisha wanahabari, wasanii na mashabiki wa burudani katika mkutano na wanahabari kuelekea shoo ya Funga Mwaka itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (2)
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akielezea jinsi walivyojipanga kwa shoo hiyo ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (3)Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akionyesha kadi ya Airtel Money Tap Tap inayomuwezesha mteja kufanya malipo mahali popote na watakaohudhuria shoo ya Diamond kununua tiketi kwa punguzo la shilingi 5000 kwa wateja 1000 wa kwanza.
Funga Mwaka Concert 2015 (4)
Mratibu wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akiongea na wanahabari pamoja na mashabiki (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuwapa burudani mashabiki siku ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (5)
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Staric ambaye naye atapanda jukwaani siku hiyo akiongea na mashabiki.
Funga Mwaka Concert 2015 (6)
Diamond akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.
Funga Mwaka Concert 2015 (18) Funga Mwaka Concert 2015 (19)
Baada ya kuongea na mashabiki wake Diamond aliamua kugawa CD na DVD za nyimbo zake kwa mashabiki waliohudhuria.
Funga Mwaka Concert 2015 (20)
Diamond akiwaaga mashabiki na kuwataka wakutane Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (21)
Mashabiki wakiwa wamemzingira Diamond wakati akiondoka eneo la mkutano na wanahabari leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (22) Funga Mwaka Concert 2015 (23)Mashabiki wakiwa wamezingira gari la Diamond wakati akiondoka.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kipenzi cha watu
    safi sana mondi watasubiri sanaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  2. Kuna kundi fulani hawataki hata kusoma habari zake,ila ndio basi tena jamaa kafunika!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad