Dk. Slaa Atoka Mafichoni 'Nadhani Sasa Mnanielewa Niliposhikilia Msimamo Wangu'

Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.

Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.

Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka, nimefurahi sana,” Dk. Slaa ameliabia gazeti la Raia Mwema.

Amesema kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amemshauri Rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua.

Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. 1.Tukisema EL asingeweza tunaambiwa usbiki tu. Lakini angeweza kweli kufichua watu wa team EL tena wengine wa ndani na karibu wa team yake (vingunge 2 wa TRA na 1 STANBIC)?
    2.Lakini ingewezekana watu wote wa nia njema bila kujali chama au historia ya chama wangeungana kuhakisha mustakabali bora wa nchi yetu. Tusije kupoteza vipaji kwa sababu ya uanachama tu au historia ya uanachama fulani.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli kama kuna kiongozi hata wa upinzani asiyeunga mkono jitihada za Magufuli lazima atakuwa na mambo yake binafsi kama sio ugonjwa wa akili.Tumuombee kwani naamini huu sio moto wa kifuu,kwa tunaomjua na kufanya nae kazi ni kwamba huyu mtu hata kama anaumwa huzuka tu kwenye sehemu ya kazi anapopata unafuu.Sasa watanzania wenzangu mnaweza pata picha huyu ni mtu wa aina gani.Tusijidanganye kwamba mbona hata awamu ya nne alianza hivi lakini baadae alipoa,kwa Magufuli hapana chezea,ni KAZI TU.

    ReplyDelete
  3. Dr slaa itabidi urudi upya ccm ili ikiwezekana upewe ukuu wa mkoa.

    ReplyDelete
  4. mzee wakuelewe ili iwe nini mbona hutulii wewe mzee unamchokoza mchumbaako masumbuzi alikukataza mambo ya siasa. hata wakikuelewa haisaidii kwa sasa ni kazi tu ndo habari ya mjini matumaini peleka monduli.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad