Exclusive: Ben Pol Aeleza Kwanini Alimuandikia Alikiba Tweet iliyozua Utata Mkubwa!

Ali Kiba na Ben Pol
Ben Pol amesema tweet ya utata aliyomuandikia Alikiba, alikusudia kumtumia kwenye ujumbe wa siri wa mtandao wa Twitter (DM) lakini akakosea na kuiweka wazi!

Juzi kupitia mtandao huo, Ben Pol alimuuliza Alikiba swali, “Bro @OfficialAliKiba mi naona kama unakuwa overrated halafu inakugharimu.. au Haikugharimu?”

Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa wasanii wamekuwa wakiambiana ukweli kuhusu muziki na maisha yao ili kuwekana sawa.

Ile tweet kwanza nilikuwa nataka iende DM,” alisema.
“Unajua sisi wasanii tunaongeaga tu, mtu anaweza akakwambia ‘mwanangu mbona hauna kiki.’ Kwahiyo mimi nilikuwa naipeleka ile tweet DM, lakini nikaipost kimakosa ikaenda public,” alifafanua.

“Mimi pale kitu kimoja kimenichanganya, watu wengine wamesema poa, wengine wanasema hapana, wengine wanatukana kwahiyo kwa kifupi hali imekuwa tafrani.

Sasa Ali alivyoona labda na yeye amelipokea vibaya baada ya kuona nimeweka public ndio maana akajibu namna ile. Kwa sababu hajanipigia akaniuliza mbona mwanangu umeandika hivi? Ila yeye aliona kama noma na iwe noma. Mimi haijanigharimu, labda kwa sababu watu wanaandika vibaya kwenye mitandao ya kijamii lakini hii ni kawaida lakini nachotaka watu wajue nilitaka tweet iende DM. Sijawahi kugombana naye, hatupo pamoja mara nyingi lakini tupo pamoja,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Ben Pol amewataka mashabiki wake kuitazama video ya wimbo wake ‘Ningefanyaje’ aliyoiachia wikiendi hii.

Source:Bongo5

Nafasi za Kazi 

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ben pol, unatafuta kiki? Maana kiukweli sijakusikia mitandaoni siku nyingi. Na Kama unasikikaga basi siku mbili tatu kwisha habari. Ila kwa hii post yako kuhusu kiba naona umedumu mtandaoni kama kawiki hivi. Jitahidi,ukitaka kusikika sana na sana mtaje Diamond na Wema, utadumu mtandaoni kama mwezi hivi sasawa.

    ReplyDelete
  2. Hi yetu macho kigoma kuna mambo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad