Mbunge wa Chalinze, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ,kwa niaba ya familia yake ametoa tamko zito kupinga tuhuma mbalimbali zinaozoelekezwa kwake na familia yake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Jana,Ridhiwani alisema baada ya Rais Kikwete kumaliza muda wa miaka 10 madarakani, baadhi ya watu wamekuwa wakiiandama familia yao kwa tuhuma mbalimbali.
Alisema baadhi ya tuhuma zinamhusisha yeye mwenyewe kwa lengo la kuupotosha uuma.
Alizitaja tuhuma hizo kuwa ni utoroshaji wa makontena kwenye bandari ya Dar es Salaam na kusisitiza kwamba tuhuma zote zinazotolewa hazina ukweli wowote bali zimelenga kumchafua yeye na familia yake.
Ridhiwani alisema tangu serikali ya awamu ya tano ianze kuwabana watu wanaokwepa kulipa kodi za serikali,baadhi ya watu wanafanya jitihada za kumhusisha na watuhumiwa hao.
Alisema hajawahi kuagiza bidhaa yoyote kutoka nje,kuwa na kontena la kulipiwa ushuru,kukwepa au kumuombea msamaha wa kupunguziwa kodi mfanyabiashara yeyote aliyeagiza kontena kutoka nje, hivyo mwenye ushahidi juu ya hilo autoe.
"Kama kuna mtu mwenye ushahidi autoe hadharani mimi niuone,dunia iuone, nawahakikishia ushahidi huo haupo na hautokuwepo labda uwe wa kughushi na wakifanya hivyo wataumbuka.
"Sina na sijawahi kumiliki lori au basi katika maisha yangu.Sina hisa wala ubia na mtu yeyote au kampuni ya malori au mabasi." Alisema Ridhiwani na kuongeza;
"Naambiwa hapa nchini siku hizi kila jengo jipya linalojengwa inasemekana ni langu na vituo vipya vya mafuta naambiwa ni vyangu.Huo ni uongo mtupu.
"Naomba nimalizie kama nilivyoanza,yanasemwa mengi lakini ni maneno ya uzandiki na uzushi mtupu usio na chembe ya ukweli.
"Wanaosema, kuandika na kueneza maneno hayo wanajua wanasema uongo isipokuwa wanafanya hivyo kwa nia mbaya dhidi yangu na familia yangu.Nawaomba watanzania muwapuuze."
Familia Ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Yatoa TAMKO Zito....Yasisitiza Haihusiki na Utoroshaji wa Makontena Bandarini.Mwenye Ushahidi Autoe
9
December 25, 2015
Tags
wasio na kazi kuandika na kusema uzushi ajira yao. kama wanasema kweli chini ya jua hakuna kinachojificha kina muda wake pengine siku arobaini kitaonekana, lakini kama ni uzushi jamani mwacheni mzee wa watu apumzike miaka 10 sio mchezo unaweza kukosea sebuse dakika 90 tu uwanjani watu hutoka jasho. kwa sasa tuendeleze zoezi la uaminifu na uadilifu kazini na kwenye biashara zetu pia.
ReplyDeleteSababu baba yako kikwete kwa kutokuwachukulia hatua mafisadi ndio maana watu tunaona na yeye anausika, sababu taalifa alikua anapewa za bandarini na sehemu zingine yeye aliuchuna, kwaiyo kuna faida alikua anapata
ReplyDeleteWa ovyoovyo wewe
ReplyDeleteMmh hapa kazi tu. Mungu mlinde Rais wetu MAGUFULI azidi kutumbua mijipu iliyooza.
ReplyDeleteMmh hapa kazi tu. Mungu mlinde Rais wetu MAGUFULI azidi kutumbua mijipu iliyooza.
ReplyDeleteMmh hapa kazi tu. Mungu mlinde Rais wetu MAGUFULI azidi kutumbua mijipu iliyooza.
ReplyDeleteHuwezi kujitetea namna hii. Heo cha mzee wako kinauwezo na kilikuwa na uwezo mkubwa sana kufanya lolote kutumia watu, makampuni na balozi nyingi tuu bila kujulikana moja kwa moja. Kawatetea wote wa ESCROW hata baada ya ya vithibitisho. Hhaya ni mLi ya umma. Kakwamisha katiba ambayo ingeweza kuthibiti ufisadi.chini ya uongozi wake haya yote ambayo Raisi Magufuli anapangua, ni mzee wako aliyalea. Kwa kiongozi yeyote kutokujua yatendekayo kama yeye hahusiki haiwezekani hata. Na huwezi kujitetea hivi kwa maneno. Hapa unazuia utendaji kazi wa magufuli na serikali mpya. Acha sheria ifuuatilie na ifanye kazi yake. Wewe ulimtuhimu Lowassa je leo.pisha magufuli na serikali ifagie nchi na jchukue hatua sawa kwa wote bila ubaguzi. Lisemwalo lipo.muna watu wanaushahidi uliofanya nao kazi. Kaa kimya sheria iheshimike na itumike sawa kwa wote na acha papara.
ReplyDeleteNanukuu:
ReplyDeleteNyerere ana watoto,
Mwinyi ana watoto,
N'kapa ana watoto,
Baba yako Mrisho,aka Tezi Dume,ana watoto wengine. Kwa nini kila kitu ni wewe tu? Au ndio habari za mkemia wa 49% wa kubambikiwa?
Familia yenu yote imeoza, sasa mnataka kujisafisha watanzania wawamini, kaeni kimya mmetuibia na kutupotezea muda kwa miaka kumi bila maendeleo ya maana wakati nchi maskini kama Ethiopia wana miundo mbinu ya maana. Kaeni kimya tunajua kazi ya baba yako ilkuwa kulinda wezi tu. Nchi hii kwa miaka kumi iliyopita ilikuwa haina raisi
ReplyDelete