Gazeti la Mwanahalisi Latoa Majina Yaliyovuja Baraza la Mawaziri wa Magufuli

Wakati joto la kusubiri rais John Magufuli atangaze majina ya baraza lake la mawaziri likizidi kupanda, gazeti la Mwanahalisi limetoa baadhi ya majina yanayodaiwa kuvuja kutoka kwenye orodha hiyo.

Mmoja kati ya majina ambayo yamevuta usikivu wa wengi ni jina la aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe ambaye alikuwa mmoja kati ya wagombea wa CCM waliokuwa wanatajwa kuwa chaguo la rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwana Halisi, majina mengine yanayotajwa ni pamoja na January Makamba,Dk. Asha Rose Migiro,Ridhiwani Kikwete,Peter Serukamba na Mwigulu Nchemba.

Jina jingine lililotajwa kwenye orodha hiyo ni jina la aliyekuwa Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), Dk. Charles Kitima.

 Dk. Kitima anadaiwa kuwa mmoja kati ya watu waliomuamini sana Dk. Magufuli wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na hata kumualika kuwa mgeni rasmi kwenye mahafari ya chuo hicho.

NB: Majina  haya  ni  kwa  mujibu  wa  gazeti  la  Mwanahalisi ambalo limedai kuyapata baada ya kuvuja. Rais Bado hajatangaza baraza lake la mawaziri

Hata hivyo,Rais Magufuli anatarajiwa kutangaza baraza lake la mawaziri muda wowote kuanzia sasa. 

Kwa mujibu wa katiba, rais anapaswa kutangaza baraza lake kabla ya kuanza kwa vikao vya bunge vya mwezi Januari.

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Oops
    Riziwan
    Mwigulu
    Nape
    Kama kweli pole rais

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmeanza wapinzani, kazi yenu ni kupinga tu kila kitu............hebu mwacheni achague awatakao, hata alipomteua MAJA pia mlichonga......msijitie kujua, MUMWACHE, HAPA KAZI TU.........

      Delete
    2. Koma wewe nipo CCM damu

      Delete
  2. Pia kipara makamba
    Anza na watu wapya kabisa

    ReplyDelete
  3. siamini hizi habari
    mpaka nisikie baraza la mawaziri toka kwa rais mwenyewe

    ReplyDelete
  4. Chaguwa mawaziri hata wapinzani watawaheshimu
    Kwa maadili yao, utendeaji wao na lugha zao kwa jamii

    ReplyDelete
  5. Natamani au ningependa ungekuwa UKAWA
    Lakini huko CCM sijui Kama utaweza

    ReplyDelete
  6. ridhiwani hapana hafai

    ReplyDelete
  7. Ukawa wapiga dili tuu muachen rais wetu msitulete siasa huu sio muda Wa siasa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sisi ni CCM
      Hatutaki mawaziri au marafiki WA Msoga hapa

      Delete
    2. wakushukuliwa ni chadema na lowasa, ndio wameleta upinzani wa kweli nchini mpaka ccm ikaufyata na kuamua kuanza na style hii.
      bila upinzani imara maccm yalikuwa yamellala mbaya. siku zote nitaunga mkono upinzani hata kama upinzani siku umechukua nchi nitaunga mkono chama ambacho kitakuwa nje ya utawala kwa ajili ya kuleta mawazo mbadala siku zote. bila chadema haya mambo tusingeyajua tungeendelea kubaki mandina wa kufa mtu

      Delete
  8. Nimependa hii,Wasukuma tunasema mchawi mpe mtoto wako akulelee.Kama kuna fisadi hapo kwenye hiyo list(kama kweli)halafu akalipa pesa zetu na akakubali kwenda na kasi ya magufuli kuna shida gani?
    Changanya baba,muweke na yule wa ACT.

    ReplyDelete
  9. Mhe, Kubenea wewe sasa ni mbunge acha uwana harakati, sasa kama kulikuwa kuna sehemu unakasoro jaribu kipindi hiki kujirekebisha. Kwa bahati mbaya unaona sasa inatakiwa kutengenezwa serikali ambayo hata nyinyi na kelele zenu hamuwezi kuijenga hata kwa miaka mia.Mnaanza kuleta mambo ya kitoto baada ya mtandao wenu uliokuwa unawapa jeuri kukatawa miguu hasa TRA na TPA, bado kwenye ofisi za serikali ambapo nyinyi ndipo kuna agents wenu wa kupata taarifa nao pia dawa yao inachemka, na uwezo wa kuwalipa hamtakuwa nao kwa hali inavyokwenda. Tafuteni muelekeo mwingine katika siasa zenu muache Dr Jpm afanye kazi.Wewe utangaza baraza la mawaziri kama nani? subiria la kwenu wakati Lowasa atakapokuwa rais 2060.ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete
  10. kufuli is looking for regitimate ya kutawala kutokana na masihara ya uchaguzi

    hakuna anaeweza kuwa juu ya tasisi wengi mtakataa lakini time will tell, kuna majumba kijiji kizima ya msauz kule chato nao ni ufisadi wake kufuli kwa ajiri ya kuwapangishia watumishi wa halmashauri ya mji sijui hamuoni hilo. seneta ya ccm inafanya kazi mbeleni wanaoshabikia watajizarau maradufu! ni mapema kukurupuka kusifia seneta ya ccm hiyo kwa wenye akili subiri bunge na baraza lianze . pia nchi haijengwi na amri na matamko tunataka kuona sharia za kijinga zote zinazosababisha hasara zinaletwa bungeni. tunataka kuona nchi inajengwa ktk mifumo sio mtu na ccm, serikali na chama visiingiliane ili kuliokoa taifa na balaa ya usoni!

    usikurupuke kutukana fikili kwanza na tazama mbali sio kama magamba! usiwe kama umetindiwa ubongo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad